Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Patagonia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rangiya njano inaonyesha eneo laPatagonia.

Patagonia ni sehemu yakusini kabisa yabara laAmerika ya Kusini yenyeumbo la pembetatu ndefu. Inajumlisha sehemu za kusini zaArgentina naChile. Iko kusini kwamtoRío Colorado ya Argentina na mtoRío Bío Bío ya Chile. Upande wamagharibi ikobahari yaPasifiki na upande wamashariki ile yaAtlantiki zinazokutana kusini kabisa katikamlangobahari wa Magellan. Kusini kwamlango bahari huo likofunguvisiwa laTierra del Fuego (nchi ya moto).

Mikoa ya Chile yaLos Lagos,Aysen naMagallanes pamoja na mikoa ya Argentina yaNeuquén,Río Negro,Chubut,Santa Cruz naTierra del Fuego katikaMkoa wa Tierra del Fuego, Antaktiki na Visiwa vya Atlantiki Kusini iko yote katika Patagonia.

Wakazi na eneo

[hariri |hariri chanzo]
  • Wakazi = 1,740,000 (sensa ya mwaka 2001).
  • Eneo =km² 900,000 pamoja na Patagonia ya Chile na Tierra del Fuego
  • Msongamano wa watu = 2.21 / km²

Jiografia

[hariri |hariri chanzo]

Sehemu kubwa ya Patagonia ya Argentina nitambarare kavu kwa sababumvua haipitimilima yaAndes.Hali ya hewa nibaridi kiasi hadi baridi.

Patagonia ya Chile inapokea mvua nyingi mlimani. Kusini penye baridi kunabarafuto kubwa.

Uchumi

[hariri |hariri chanzo]

Migodi nauvuvi baharini ni muhimu. Katika nchi kavu ya kusini kunaufugaji wakondoo.Kaskazini kunakilimo.

Picha

[hariri |hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo yaAmerika Kusini bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuPatagonia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Patagonia&oldid=1288379"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp