Inahesabiwa kuwa sikukuu muhimu kabisa katikamadhehebu mengi yaUkristo, kwa sababu ufufuko huo ndio msingi waimani ya Kikristo.Mtume Paulo aliandika kwambaKristo asingefufuka, imani hiyo ingekuwa haina maana, kwa kuwa asingeondoleadhambi za watu.
15:1 Basi, ndugu zangu, nawaarifu ile injili niliyowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama, 2 na kwa hiyo mnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri isipokuwa mliamini bure. 3 Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; 4 na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko; 5 na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Thenashara; 6 baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala; 7 baadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote; 8 na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake. 9 Maana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mitume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu. 10 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami. 11 Basi, kama ni mimi, kama ni wale, ndivyo tuhubirivyo, na ndivyo mlivyoamini.
12 Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu? 13 Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka; 14 tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure. 15 Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi. 16 Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka. 17 Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu. 18 Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea. 19Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote.
20 Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. 21 Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. 22 Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa. 23 Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja. 24 Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. 25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. 26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti. 27 Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo. 28 Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.
Etimolojia
Jina la "Pasaka" limetokana nasherehe yaPasaka ya Kiyahudi linaloitwa "פסח" (tamka: pasakh) kwalugha yaKiebrania. Kinyume chaKiingereza, ambacho kina maneno mawili,Passover naEaster, katikaKiswahili na lugha nyingine nyingi majina ya sherehe za Kikristo na Kiyahudi hazitofautiani.
Asili yake ni kwamba kusulibiwa na kufufuka kwaYesuKristo kumetokea wakati wa sikukuu ya Pasaka ya Kiyahudi mnamoAprili yamwaka30BK.
Wakristo wa kwanza, ambao wote walikuwa Wayahudi, walisheherekea sikukuu ya Kiyahudi pamoja na kumbukumbu yaufufuko wa Yesu. Baadaye sherehe na piatarehe zikawa tofauti, ingawa bila kwenda mbali sana. Badiliko kubwa zaidi lilikuwa lile la Wakristo kuadhimisha daima Pasaka siku ya Jumapili kwa kuwa ndiyo siku ya ufufuko, wakati Wayahudi wanadhimisha Pasaka kwa kuangalia tarehe, bila kujali ni siku ipi ya juma.
Tarehe ya Pasaka
Tarehe za Pasaka kwa miaka 2000-2040 (Tarehe zote zinaonyeshwa kufuatana na kalenda ya Gregori)
Katikakalenda ya kawaidatarehe ya Pasaka inabadilika kilamwaka, ila inapatikana katikaMachi auAprili tu, kwa sababu upande mmoja inafuata kuonekana kwamweziangani, lakini imefungwa pia kwasikusare (au ekwinoksi, yaani siku ya usawa wamchana nausiku), kwa hiyo haizunguki mwaka mzima kama tarehe za sherehe zaUislamu.
Wakristo wa kwanza, ambao wote walikuwa Wayahudi, walisherehekea sikukuu ya Kiyahudi pamoja na kumbukumbu ya ufufuko wa Yesu. Baadaye sherehe na pia tarehe zikawa tofauti, ingawa bila kwenda mbali sana.
Badiliko kubwa zaidi lilikuwa lile la Wakristo, tangukarne ya 1 auya 2, kuadhimisha daima Pasaka siku yaJumapili kwa kuwa ndiyo siku ya ufufuko, wakati Wayahudi wanaadhimisha Pasaka kwa kuangalia tarehe, bila kujali ni siku ipi yajuma.
Mtaguso wa kwanza wa Nisea mwaka325 uliamua kwamba Pasaka isherehekewe Jumapili ya kwanza baada ya mwezi mpevu wa kwanza unaofuata tarehe 21 Machi. Kwa kuwa mwezi mpevu baada ya 21 Machi inaweza kutokea kati ya 22 Machi na 19 Aprili, tarehe ya Pasaka, ambayo ni Jumapili inayofuata, hutokea kati ya22 Machi na25 Aprili.
Katika Ukristo kuna kalenda mbili zinazotumika, hivyo pia tarehe mbili za Pasaka.Kanisa la magharibi, yaaniWakatoliki wengi naWaprotestanti, hufuatakalenda ilivyorekebishwa naPapa Gregori XIII (ambayo imekuwa kalenda ya kawaida ya kimataifa), lakiniWaorthodoksi wanaendelea kutumia kalenda iliyotangulia, yaaniKalenda ya Juliasi. Ndiyo maana mara nyingi Pasaka inaadhimishwa katika Jumapili tofauti kati ya pande hizo mbili: tofauti ya kalenda inaletaKanisa la Mashariki kusheherekea Pasaka wakati mwingine hata katika mweziMei wa kalenda ya Gregori, kwa kuwa kwao bado ni Aprili kufuatana na kalenda ya Juliasi.
Kwa sasa kuna majadiliano yenye lengo la kukubaliana ili kuadhimisha Pasaka pamoja kama ilivyokusudiwa na Mtaguso wa kwanza wa Nisea.
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Maurice Soseleje, Kalendari yetu – Maisha ya Watakatifu – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1986 –ISBN 9976-63-112-X, uk. 34-35
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuPasaka ya Kikristo kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.