Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Parokia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sehemu ya mfululizo kuhusu
Ukristo
Yesu Mchungaji mwema.


Parokia ni muundo mmojawapo wa zamani sana waKanisa Katoliki, ambao umuhimu wake unatokana na kwamba ni sehemu yajimbo (dayosisi) unapofanyikauchungaji wa kilasiku chini yakasisi anayemwakilishaAskofu.

Kiini chamaisha ya parokia niadhimisho laEkaristi siku yaJumapili, ambapojumuia nzima yaKikristo ya eneo husika inakusanyika isikilizeNeno la Mungu, imsifuMungu naKumega mkate.

Jina

[hariri |hariri chanzo]

Jina hilo lilianza kutumika katikakarne III kutokana naneno laKigiriki παρоικια (=ujirani) linalotumika katikatafsiri yaBiblia yaSeptuaginta kwa maana yakukaa ugenini.

KatikaSheria za Kanisa Katoliki

[hariri |hariri chanzo]

Kanuni 515 zaSheria za Kanisa la Kilatini inasema, "Parokia nijumuia rasmi ya waamini ambayo imeundwa kwa namna ya kudumu ndani yaKanisa maalumu na imekabidhiwa kichungaji kwaparoko kamamchungaji wake chini yamamlaka yaAskofu wa jimbo. Ni juu ya Askofu wa jimbo tu kuanzisha, kufuta na kubadilisha parokia; lakini asizianzishe, asizifute wala asizibadilishe sana kabla hajapokea maoni yaHalmashauri ya mapadri. Parokia iliyoundwa kihalali papo hapo inahadhi yanafsi ya kisheria".

Katikamadhehebu mengine

[hariri |hariri chanzo]

Mbali yaKanisa Katoliki, ambalo linamtandao mkubwa zaidi wa parokiaduniani kote,Waorthodoksi,Waanglikana,Walutheri naWakristo wengine kadhaa wanatumia muundo wa namna hiyo, ingawa mikazo ni tofauti, kulingana nateolojia yao.

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuParokia kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Parokia&oldid=1051328"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp