Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Papa Viktor I

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Papa Vikta I katikadirisha lakioo cha rangi (Semmering,Austria).

Papa Viktor I (auVictus I) alikuwaPapa kuanzia takriban186/189 hadikifodini chake takriban197/201[1].

AlimfuataPapa Eleutero akafuatwa naPapa Zefirini.

Alikuwa Papa wa kwanza kutokeaAfrika, labdaLeptis Magna, leo nchiniLibya.

Anajulikana hasa kwa msimamo wake mkali kuhususuala la tarehe ya Pasaka, wakati kabla ya yeye kufanywa Papa, tofauti kuhusutarehe hiyo haikusababishafarakano.[2] Kwa kuwa alitenga naKanisa walioadhimishaPasaka ya Kikristosiku moja kabla yaPasaka ya Kiyahudi, siJumapili iliyoifuata kama hukoRoma[3],Ireneo na wengineo walimlaumu, kadiri alivyoandikaEusebi wa Kaisarea.

Hata hivyo, tangu kale anaheshimiwa kamamtakatifumfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe28 Julai[4].

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Maandishi yake

[hariri |hariri chanzo]

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  2. "Philip Schaff: NPNF2-01. Eusebius Pamphilius: Church History, Life of Constantine, Oration in Praise of Constantine - Christian Classics Ethereal Library".www.ccel.org. Iliwekwa mnamo2022-01-20.
  3. https://www.santiebeati.it/dettaglio/90137
  4. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001,ISBN 8820972107

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
karne ya 1 hadi ya 4
karne ya 5 hadi ya 8
karne ya 9 hadi ya 12
karne ya 13 hadi ya 16
karne ya 17 hadi ya 20
karne ya 21
Makala hii kuhusu Papa fulani bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuPapa Viktor I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuiongezea habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Papa_Viktor_I&oldid=1323843"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp