Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Papa Pius X

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Pius X.

Papa Pius X (Riese,Veneto,Italia Kaskazini,2 Juni1835Roma,20 Agosti1914) alikuwaPapa kuanziatarehe4/9 Agosti1903 hadikifo chake[1]. AlitokeaRiese,Treviso,Italia[2].

Jina lake la kuzaliwa lilikuwaGiuseppe Sarto.

AlimfuataPapa Leo XIII na kuvishwataji la Kipapa tarehe9 Agosti1903, wa kwanza katikakarne ya 20. Akafuatwa naPapa Benedikto XV.

Alitangazwa naPapa Pius XII kuwamwenyeheri tarehe3 Juni1951, halafumtakatifu tarehe29 Mei1954.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe21 Agosti[3].

Maisha

[hariri |hariri chanzo]

Kabla ya kuchaguliwa kama Papa, aliwahi kuwaparoko,askofu waMantova (tangu1884, halafuPatriarki waVenice (tangu1893). Hivyo alikuwa na mang'amuzi mengi yakichungaji.

Kwa kuwa katikauchaguzi makardinali walimpigakura kwanza mwenzao Rampolla, lakini huyo aliwekewa kura yaturufu naKaisari waAustria-Hungaria, mara alipochaguliwa Pius X alifutahaki hiyo ya Kaisari na kuamua atengwe naKanisa Katoliki yeyote atakayeingilia tena uchaguzi wa Papa.

Lengo lake lilifafanuliwa nakaulimbiu yake: "Instaurare omnia in Christo", yaani "Kukamilisha yote ndani yaKristo". Alilitekeleza kwaunyofu,ufukara nanguvu, akihamasishamaisha yaKikristo kati ya waumini kwa kuwapa nafasi ya kushiriki zaidiekaristi takatifu, kwa kustawishaubora waliturujia na kwa kuhakikishausahihi waimani[4].

Kweli alijitahidi kuleta hali mpya katikaKanisa.

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  2. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  3. Martyrologium Romanum
  4. https://www.santiebeati.it/dettaglio/24100

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
karne ya 1 hadi ya 4
karne ya 5 hadi ya 8
karne ya 9 hadi ya 12
karne ya 13 hadi ya 16
karne ya 17 hadi ya 20
karne ya 21
Makala hii kuhusu Papa fulani bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuPapa Pius X kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuiongezea habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Papa_Pius_X&oldid=1334610"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp