Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Panonia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ulaya ya Mashariki-Kusini wakati wa Roma ya Kale - Panonia iko upande wa kushoto juu yenye mipaka yarangi yakijani.

Panonia (kwa KilatiniPannonia) ilikuwajimbo laDola la Roma kuanziamwaka9 KK hadi433. Eneo lake lilipakana namilima yaAlpi upande wamagharibi namto Danubi upande wakaskazini namashariki. Leo hii eneo lake lakaliwa naHungaria ya magharibi,Burgenland yaAustria na sehemu zaKroatia,Serbia naSlovenia.

Wakati waRoma ya Kale jimbo liligawiwa mara mbili na mwaka433 lilikabidhiwa kwa mfalmeAttila waWahunni.

Wakazi

[hariri |hariri chanzo]

Leo hii sehemu kubwa hukaliwa naWahungaria lakini mababu wao waliingia hukukarne nyingi baada ya Attila. Wakati wa Waroma wakazi wengi walikuwa Wapanoni, waliokuwakabila lenyeasili kati yaWakelti. Baadaye viliingia vikundi vingi, hasa wakati waUhamisho mkuu wa Ulaya katikakarne ya 3 hadiya 10.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Waroma wa Kale walienezamilki yao huku chini yakaisariAugusto aliyesukuma mpaka wa Dola la Roma hadi mto Danubi. Mwaka6BKwazalendo walijaribu kuwafukuza Waroma lakini walishindwa na mwaka9 jimbo la Panonia liliundwa. Waroma walijengamaboma mengi kando ya mto Danubi kama vituo vyaulinzi dhidi ya makabila makatili yaliyokalia upande mwingine wamto huo.

Katikakarne ya 5 nguvu ya Dola la Roma ilififia mbele ya mashambulio ya makabila mengi kutoka mashariki na kaskazini. Mfululizo wavita mbalimbali uliharibu nchi na wakazi wengi Waroma waliondoka wakahamia sehemu zenyeusalama zaidi. HivyoKaisariThedosio II aliondoalegioni zake kutoka Panonia akakabidhi nchi yote kwa Wahunni chini yamfalme Attila.

Baada yakifo cha Attilautawala wa Wahunni ukaporomoka namakabila ya Kigermanik yalitawala yakifuatwa naWaslavi mbalimbali.

Tangu mwaka900 Wahungaria walifika wakaanza kutawala nchi na wakazi wengi polepole wakapokealughayao.

Baadayewatawala waHabsburg kutoka Austria naWaislamu waMilki ya Osmani walishindania utawala wa eneo lililokuwa sehemu ya Milki yaAustria-Hungaria hadi1918. Mwaka huo eneo likagawiwa kwa Austria, Hungaria na Ufalme waYugoslavia.

Makala hii kuhusu maeneo yaUlaya bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuPanonia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Panonia&oldid=1358378"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp