| Outkast |
|---|

Outkast kutoka 2001 |
| Maelezo ya awali |
|---|
| Asili yake | Atlanta naSavannah Georgia,Marekani |
|---|
| Aina ya muziki | Hip hop,Dirty South,G-Funk |
|---|
| Miaka ya kazi | 1990- |
|---|
| Studio | Laface Records |
|---|
| Ame/Wameshirikiana na | Dungeon Family,Purple Ribbon All-Stars,T.I.Sleepy Brown,Goodie Mob,Witchdoctor,Organized Noize,UGK,Raekwon |
|---|
| Tovuti | http://www.outkast.com |
|---|
| Wanachama wa sasa |
|---|
Antwan "Big Boi" Patton "André 3000" Benjamin |
Outkast auOutKast ni kundi lamuziki wa hip hop lenye makazi yake huko mjiniEast Point, Georgia nchiniMarekani. Kundi linaunganishwa na watu wawili, ambao niAndré "André 3000" Benjamin naAntwan "Big Boi" Patton. Kundi lilianzishwa mnamo mwaka wa 1990.Awali walikuwa wakijulikana kama The OKB (The OutKast Brothers) lakini baadaye wakabadilisha jina la kundi na kuwa OutKast. Mtindo wa uimbaji wa zamani wa kundi hili ilikuwa mchanganyiko waDirty South naG-Funk.[1] Tangu hapo, lakini,funk,soul,electronic music, ushairi wa kutamka maneno,jazz, na elementi zablues zimekuwa zikiwekwa kwenye muziki wao.[2][3]
Wawili hawa ni moja kati ya makundi ya hip-hop yenye mafanikio kwa muda wote, kwa kupokea tuzo sita zaGrammy Awards. Zaidi ya nakala milioni 25 zimeuzwa kwenye matoleo nane ya albamu za OutKast: albamu za studio sita, toleo lavibao vikali, na albamu ilioshinda tuzo ya Grammy Award-ikiwa kama (Albamu Bora)Speakerboxxx/The Love Below, albamu ya pamoja iliyojumlisha albamu moja-moja kutoka kwa kila mwanachama.