Olso iko kwenye mwisho wa kaskazini wafyord ya Oslo (fyord ni jina la hori ndefu na nyembamba za pwani la Norwei). Visiwa 40 ni sehemu ya eneo la mji. Mahali pa juu ni mlima wa Kirkeberget mwenye kimo cha mita 629. Kuna misitu mingi ndani ya eneo la mji huu.
Kumbukumbu za Norwei ziandai ya kwamba mji uliundwa na mfalmeHarald III manmo mwaka 1048 lakini wataalamu waakiolojia wamekuta makaburi ya kikristo yanayotangulia tarehe hii.
Jengo mashuhuri la mji ni boma la Akershus lililojengwa kuanzia mwaka 1290.
Mji ulichomwa na moto mnamo 1624. Ulipojengwa upya kwa amri wa mfalmeChristian IV ikapewa jina la "Kristiana" (Mji wa Christian). 1925 jina la Oslo likarudishwa.
Makala hii kuhusu maeneo yaNorwei bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusuOslo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.