Oksijeni (en:oxygen) nielementisimetali yenyenamba atomia8 nauzani atomia 15.9994 kwenyemfumo radidia.Alama yake niO.
Ni kati ya elementi zilizopo kwa wingiulimwenguni ikishika nafasi ya tatu baada yahidrojeni naheli. Kwenyedunia yetu asilimia 28 zamasi yake ni oksijeni; ni elementi iliyopo kwa wingi kabisa katikaganda la dunia.
Hutokea ama kama mchanganyiko wa elementi nyingine au pekee yake kamagesi isiyo na rangi wala herufi. Pekee yake hupatikana hasa kamamolekuli ya O2 yaani mchanganyiko wa kikemia waatomi mbili. Kuna pia oksijeni ambayo ni molekuli ya atomi tatu unaoitwaozoni (O3).
Umuhimu wake duniani ni hasa kuwepo katikamaji na katikahewa yaangahewa na kwa ujumla kwa ajili ya uhai. Karibu viumbe vyote duniani hutegemea oksijeni. Wanaipata ama kwa kupumua hewani au kwa kuichukua kwenye maji. Oksijeni tupu ni sumu kwa ajili ya viumbe vingi.
Kama atomi ya pekee ya oksijeni inakutana na atomi mbili zahidrojeni zinakuwa H2O (maji).
Gesi ya oksijeni hutumiwa sana katika teknolojia mbalimbali. Kwa sababu mwendo wa kuchoma huhitaji oksijeni inatumiwa pale ambako jota inatakiwa, kwa mfano wakati wa kuchomelea inapochanganywa na gesi yaasetilini.
Vile hutumiwa katikaroketi. Injini zote zapetroli audiseli huhitaji oksijeni lakini kwa kawaidi zaichukua hewani tu. Oksijeni tupu ina hatari yake kwa sababu yaweza kusababisha mlipuko ikikutana na moto.
Hutengenezwa kwa njia mbalimbali hasa kwaelektrolisisi ya maji kuwa gesi ya O2 na H2.Inapatikana pia kwa kuvunjakabonati ya kalsi (CaCO3) kuwa CaO na O2.
Mimea hupata mahitaji yao ya oksijeni katikachanikiwiti kutokana na CO2 namaji kwa nishati ya mwanga wa jua kuwa O2 na C6H12O6 inayojenga molekuli mpya zaselulosi.
Oksijeni ina sifa mbalimbali ambazo huweza kuwa za kawaida ama za kikemikali. Sifa hizo ni kama vile
- Oksijeni huyeyuka kidogo sana katikamaji.
- Oksijeni nigesi yenyedensiti kubwa kuliko ile yahewa.
- Oksijeni haina hatua yoyote katikamaji ya chokaa.
- Oksijeni inasaidia mwako. Ukiweka njiti yakiberiti inayokaribia kuzima kwenye chombo chenye gesi ya oksijeni, njiti hiyo itaendelea kuwaka.
- Oksijeni ni gesi isiyokuwa naharufu,rangi walaladha yoyote ile.
- Oksijeni huchanganyika namadini au metali zisizo zasumu ili kuundaoksidi ya metali auoksidi zisizo zametali.
 | Makala hii kuhusu mambo yakemia bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuOksijeni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari. |