Nyuki-asali hufugwa sana kila mahali duniani lakini wengine wanaishi porini na asali yao hukusanywa kwa kuvunja mizinga yao. KatikaAfrika kwa jumla sehemu ya asali bado inatokana na nyuki asali wa porini lakini ufugaji nyuki unaendelea kupanuka.
Nyuki-asali ni wadudu wa kijamii maana yake wanaishi katika makundi si peke yao kama aina nyingine za nyuki. Wanajenga sega ya nta ndani yamzinga wa nyuki na humu hutunza asali yao.
Kuna aina tatu za nyuki ndani ya kundi hili nao ni:
malkia wa nyuki ni mama wa nyuki wote ndani ya kundi na kazi yake ni kutaga mayai pekee
nyuki wafanyakazi ni wakazi wengi wa mzinga na wote ni wa kike. Ni hao wanaofanya kazi yote kama kukusanya mbelewele na mbochi, kusafisha mzinga, kutengeneza nta, kujenga sega, kumlisha malkia na majana, kulinda mzinga
nyuki wa kiume auwadudume ni wachache na kazi yao ya pekee ni kumpanda malkia ambaye si yule wa mzinga wake kwa kawaida; baadaye wanafukuzwa kwenye mzinga na hawapewi chakula tena
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuNyuki-asali kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.