Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Nusuranyota

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya sanaa ya kisahani cha uongezekaji cha nusuranyota.

Nusuranyota (kwa kiingereza:quasar) nikiini angavu sana cha majarra hai. Nguvu yamnururisho wake inatokana nashimo jeusi la tungamomno, lenyetungamo kutokatungamo ya Jua milioni kumi hadi bilioni kumi, na huzingirwa nakisahani cha uongezekaji. Kuanguka kwagesi ya kisahani hupashajoto na hutoanishati yenye jinsi yamnururisho sumakuumeme. Nishati ng’avu ya nusuranyota ni kubwa mno; nusuranyota zenye nguvu zaidi zina mng’aro maelfu ya mara mkubwa kulikomajarra kamaNjia Nyeupe.[1][2] Nusuranyota huainizishwa kama kijamii cha jamii kubwa zaidi ya kiini cha majarra hai.Misogeo miekundu ya nusuranyota inatokana nakuvimba kwa Ulimwengu.[3]

Istilahinusuranyota ni ambatani yanusura nanyota. Kwa kiingereza,quasar ni mkato wa “quasi-stellar radio source”—kwa sababu zilitambuliwa kwanza wakati wa miaka ya 1950 kama violwa vya asili isiyojulikana ambavyo hutokezamawimbiredio—na zilipochunguzwa kwa masafa wa mawimbi yanayoonekena, zilifanana na nukta dhaifu ya nuru kama nyota. Taswira zamwonekano wa juu za nyota, hasa kutokaDarubini ya Angani ya Hubble, zimeonyesha kwamba nusuranyota ziko katika vitovu vya majarra, na majarra nyinginezinaingiliana sana auzinachanganyana.[4]

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. Wu, Xue-Bing; na wenz. (2015). "An ultraluminous quasar with a twelve-billion-solar-mass black hole at redshift 6.30".Nature.518 (7540): 512–515.arXiv:1502.07418.Bibcode:2015Natur.518..512W.doi:10.1038/nature14241.PMID 25719667.S2CID 4455954.
  2. Frank, Juhan; King, Andrew; Raine, Derek J. (Februari 2002).Accretion Power in Astrophysics (tol. la Third). Cambridge, UK: Cambridge University Press.Bibcode:2002apa..book.....F.ISBN 0521620538.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Quasars and Active Galactic Nuclei".ned.ipac.caltech.edu. Iliwekwa mnamo2020-08-31.
  4. Bahcall, J. N.; na wenz. (1997)."Hubble Space Telescope Images of a Sample of 20 Nearby Luminous Quasars".The Astrophysical Journal.479 (2): 642–658.arXiv:astro-ph/9611163.Bibcode:1997ApJ...479..642B.doi:10.1086/303926.S2CID 15318893.
Makala hii kuhusu mambo yasayansi bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuNusuranyota kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Nusuranyota&oldid=1369900"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp