Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Norwei

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kongeriket Norge
Kongeriket Noreg

Ufalme wa Unowe
Bendera ya UnoweNembo ya Unowe
BenderaNembo
Kaulimbiu ya taifa: Alt for Norge ("Yote kwa Unowe" ni wito wa kifalme)
Kiapo kufuatana na katiba ya1814 : "Enige og tro tilDovre faller" ("Pamoja na waaminifu hadi milima ya Dovre inaporomoka")
Wimbo wa taifa:Ja, vi elsker dette landet

Wimbo wa kifalme:Kongesangen
Lokeshen ya Unowe
Mji mkuuOslo
59°56′ N 10°41′ E
Mji mkubwa nchiniOslo
Lugha rasmiKinowe1
(Bokmål naNynorsk)
SerikaliUfalme wa kikatiba
Harald V
Jonas Gahr Støre
Katiba
Uhuru
Ilitangazwa
Ilitambuliwa

Kutoka maungano naUswidi
7 Juni1905
26 Oktoba1905
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
385,207 km² (ya 673)
{{{percent_water}}}
Idadi ya watu
 -2025 kadirio
 -2013 sensa
 - Msongamano wa watu
 
5,594,340[1] (ya 116)
5,136,700
14.5/km² (ya 213)
FedhaKrone ya Unowe (NOK)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD.no2
Kodi ya simu+47

-

1Lugha rasmi ya Kinowe inapatikana kwa namna mbili:bokmål zaidi kama lugha ya kimaandishi naNynorsk zaidi kama lugha ya majadiliano ingawa inaandikwa pia. Lugha yaKisami ni lugha rasmi katika miji 6 naKifini katika mji mmoja.


Unowe (auːNorwe,Norwei; kwaKinorweiNorge/Noreg;jina rasmi niUfalme wa UnoweːKongeriket Norge kwaBokmål naKongeriket Noreg kwaNynorsk) ni nchi yaSkandinavia katikaUlaya ya Kaskazini.

Imepakana hasa naUswidi, ila katikancha yakaskazini naUfini naUrusi pia.

Inapwani ndefu kwenyeBahari ya Kaskazini na yaAtlantiki.

Visiwa vyaSvalbard naJan Mayen katikabahari ya Aktiki ni maeneo ya Norwei.

Pia visiwa visivyokaliwa nawatu vyaBouvet katika Atlantiki ya kusini naPeter I katikaPasifiki ya kusini viko chini ya Unowe.

Nchi inadai pia sehemu yaQueen Maud Land katikabara laAntaktika penye kituo cha kisayansi chaTroll.

Mkuu wake kwa sasa niMfalme Harald V.

Bunge huitwaStortinget na wanachama wake huchaguliwa na wananchi kila baada ya miaka minne.

Sikukuu yataifa ni tarehe17 Mei, ambapo husherekewakatiba ya Unowe yamwaka wa1814.

Miji

[hariri |hariri chanzo]

Mji mkuu niOslo, wenye wakazi wanaozidi 530,000.Miji mingine mikubwa ni pamoja naBergen wenye wakazi 230,000 naTrondheim wenye wakazi 150,000; yote miwili imewahi kuwa miji mikuu ya Unowe katika miaka ya mwanzoni.[2]

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Nchi ilikaliwa nawatuwawindaji-wakusanyaji tangu mwaka10000 KK hivi.

Katika miaka3000 -2500 KK waliingiawakulima waKizungu.

Katikakarne ya 8 hadikarne ya 10 Norwei ilipelekamabaharia wakeWaviking hadi mbali sana.

Kwa muda mrefu Norwei ilibaki katikamuungano naUdani naUswidi.

Ufalme umekuwa huru tangu mwaka wa1905.

Uchumi

[hariri |hariri chanzo]

Unowe ilikuwanchi maskini yawakulima nawavuvi, lakini tangu kupatikana kwamafuta yapetrolibaharini imekuwa kati yanchi tajiri kabisa duniani.

Watu

[hariri |hariri chanzo]

Takriban watu milioni 5.5 wanaishi nchini Unowe. Wengi wao (81.5%) ni Wanorwei asili,jamii yaWajerumani.Asilimia 18.5 niwahamiaji auwatoto wa wahamiaji wawili (hasaWapolandi,Walithuania,Wasomali,Wapakistani naWaswidi). Wengi wao sasa wanauraia wa Norwei.

Dini ya kwanza niUkristo (74.9%), hasamadhehebu yaKilutheri (68%), halafuWakatoliki (3.1%, hasa wenyeasili yaPolandi). Hata hivyo wananchi wengi hawajali sana; wanaoshirikiibada kilawiki ni 2% tu.

Katika dini nyingine, unaongozaUislamu (3.1%) ulioletwa nawahamiaji kutoka nchi mbalimbali walioongezeka sana kuanzia miaka ya mwisho yakarne ya 20. 21.2% hawana dini yoyote.

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. "Population, 2025-01-01" (kwa Kiingereza). Statistics Norway. 2025-02-25. Iliwekwa mnamo2025-02-26.
  2. "Trondheim - the official website". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2009-06-08. Iliwekwa mnamo2009-09-04.

Viungo vya Nje

[hariri |hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Search Wikinews Wikinews has related news:Norway
OpenStreetMap has geographic data related to:Norwei
Makala hii kuhusu maeneo yaUlaya bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuNorwei kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Nchi huru
Nchi zisizokubaliwa
na umma wa kimataifa
Maeneo yanayojitawala
chini ya nchi nyingine
1 nchi yaAsia ya Magharibi kijiografia ambayo huhesabiwa kuwa sehemu yaUlaya kiutamaduni2nchi ya kimabara
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Norwei&oldid=1405161"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp