Jina lake (kwaKiebraniaנחNoah, kwaKiarabuنوحNuhu) linatafsiriwa naKitabu cha MwanzoMfariji, lakini maana ya hakika zaidi niAnayeendeleza ubinadamu baada ya gharika.
Meli ya Nuhu, Zubdetü't-Tevarih. Kulingana na wasomi huria, hadithi ya mafuriko yaGilgamesh imekopwa kutoka kwaWababeli na kutafsiriwa tena katikaTorati na katikaQuran.[1][2][3]
Simulizi la gharika ni miongoni mwa yale yanayojulikana sana katika Biblia.
Katika simulizi hilo, Nuhu alifanyakazi kwauaminifu ili kujenga safina kwaamri ya Mungu, ambamo hatimaye kuokoafamilia yake nawanyama wote wa nchi kavu. Mungu aliigharikishaDunia baada ya kusikitika kwamba ilikuwa imejaadhambi.
Mwa 6:5-9:17 inatufundisha kwamba Mungu anachukizwa na dhambi, hivyo anataka kuondoa maovu duniani ili nchi impendeze kama alivyokusudia alipoiumba. Kwa ajili hiyo zamani za Nuhu aliletamaji yafunikedunia na kuzamisha waovu. Lakini alisalimisha waadilifu katika safina kubwa ya kutosha, halafu akafunga naoagano thabiti (Eb 11:7).
Kadiri yaMtume Petro maji yanayokusudiwa kutakasa dunia yote ni yale yaubatizo (1Pet 3:17-22), na safina ambayo iokoe watu niKanisa, ambalo kadiri yaAgano Jipya ni la lazima kwawokovu kama vile ubatizo unaotuingiza ndani yake.
Njiwa akaonekana tena juu ya maji siku ya ubatizo waYesu ambapo alipakwaRoho Mtakatifu na kuyatia maji nguvu ya kutakasa watu (Mk 1:9-11;Tito 3:3-7). Maji na mafuta ndiyo mwanzo mpya kwabinadamu.
Mara alipotoka safinani Nuhu alimtolea Mungusadaka iliyompendeza hata akaahidi hataangamiza tena binadamu kila anapostahili. Sadaka hiyo ni mfano wa ile ya Yesu msalabani, inayoadhimishwa katikaekaristi, ikituondolea adhabu nyingi na kutuletea huruma ya Mungu, yaani nafasi na neema ya kutubu (Tito 2:11-14). Hatimaye kutakuwa nahukumu itakayobagua waadilifu na waovu kama siku za Nuhu (Math 24:37-41).
Kwa namna hiyo, Mungu alifanyaagano na Nuhu na kuahidi kutoharibu tena viumbe vyote vya Dunia kwa gharika.
Nuhu pia anaonyeshwa kama "mkulima wa udongo" aliyelimamzabibu, pia mnywaji wazabibu hiyo. (Mwanzo 9:20-21)
Baada ya gharika, Mungu anaamuru Nuhu na wanawe: “zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi”.[4]
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuNuhu kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.