Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Njia ya Pwani ya Welisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chepstow, njia inapoishia.
Mwanzo na mwisho wa Njia ya Pwani ya Welisi.

Njia ya Pwani ya Welisi (kwaKiingereza:Wales Coast Path, kwaKiwelisi:Llwybr Arfordir Cymru) ni njia yamatembezi marefu kwamiguu inayozungukapwani yote yaWelisi. Njia inaanziaQueensferry,kaskazini mwa nchi ikiendelea hadiChepstow (Kiwelisi: Cas-gwent)kusini mwa nchi.

Urefu wake nikilometa 1,400.[1] Njia ilifunguliwa rasmitarehe5 Mei2012, ila sehemu fulani kama Njia ya Pwani pa Ziwa ya Anglesey na Njia ya Pwani pa Pembrokeshire zilitanguliwa kufunguliwa. Njia inapitia Hifadhi za Taifa mbili, Maeneo Mazuri ya Urembo matatu na Hifadhi za Asili za Kitaifa 11.[2]

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. firstnature.com - Countdown to the Wales Coast Path Ilirejewa 10 Julai 2012.
  2. bbc.co.uk - Wales Coast Path officially opens with events in Cardiff, Aberystwyth and Flint Ilirejewa 10 Julai 2012.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Njia_ya_Pwani_ya_Welisi&oldid=1406716"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp