Nikotini nidutu yaalkaloidi katikamimea mbalimbali (hasamtumbaku) ambayo nidawa linaloathirineva zamwanadamu. Matumizi yake ni hasa katikasigara, lakini pia katikakemikali namadawa.
Kuanzia kiasi fulani nisumu kali, kwa viwango vidogo inaamshaneva za watu.Hatari yake kwa mwanadamu ni hasa uzoefu unaotokea na kugeuka harakauraibu unaotawalamwili naakili kwahamu ya kurudia matumizi ya nikotini. Katika sifa hii inafanana namadawa ya kulevya hata kama kiwango cha kumwamsha mtu haufikii hali yaulevi wa namna yoyote.
Jina la dawa linatokana na jina la kitaalamu la mtumbaku "Nicotiana tabacum" na hili lilitokana naJean Nicot de Villemain aliyekuwabalozi waUfaransa nchiniUreno katikakarne ya 16. Alijipatia mbegu za mtumbaku wakati mmea huu ulikuwa umeingiaUlaya kutokaAmerika akazitumaParis kwautafiti. Ndiye mtu wa kwanza kuletambegu yamtumbaku nchini Ufaransa.
Dawa ya nikotini ndani ya majani ya mmea liligunduliwa nawanakemiaWajerumanimwaka1828.
Matokeo ya kimwili ya nikotini kwa kiwango kidogo ni kuharakisha pigo lamoyo na kupandishakanieneo ya damu. Sifa hii inatafutwa na watu wakisema matumizi yatumbaku husaidia kuondoa au kupunguzauchovu na kuamshaubongo. Lakini uamsho huu haudumu muda mrefu na mtu anapaswa kuongeza nikotini mara nyingi kwa kuvutasigara nyingine.
Hatari hasa ya dawa lenyewe ni uraibu wa hatari ya kutawaliwa nayo.
Kwa viwango kikubwa zaidi hatari zake kama sumu ya neva ni muhimu. Kiwango chamiligramu moja ya nikotini kwakilogramu moja yauzani wa mtu kinatosha kumwua mtu. Yaani mtu mwenye uzani wakg 70 hufariki akiingiza miligramu 70 mwilini. Hapa ni kwa mfano hatari yawatoto wadogo kula sigara bila kujijua: sigara moja huwa na miligramu 10 za nikotini. Mvutaji anaingiza sehemu yake tu kwa njia yamoshi lakini mlaji anapata yote na mtu mdogo huwa hatarini kabisa.
Nikotini ni kati ya sumu kali kabisa, hivyo imetumiwa kama dawa lawadudu kwa sababu mimea haina matatizo nayo, niwanyama tu. Lakini nchi nyingi zimepiga marufuku matumizi haya kutokana na hatari kwa watu wanaotumia dawa au wanaoishi katikamazingira ambako inatumiwa.
Hasara za nikotini katika sigara zinaenda sambamba na kemikali zinazokuja pamoja nayo katika sigara kama njia kuu ya kutumia nikotini. Hapawataalamu hawana uhakika kiasi ganimagonjwa yanayoonekana kati ya wavutaji husababishwa na nikotini hasa au na nikotini pamoja na kemikali nyingine ndani ya moshi.
Hasara zilizotazamwa ni kama vile:
 | Makala hii kuhusu mambo yakemia bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuNikotini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari. |