Machiavelli anajulikanaduniani kwamaandishi yake ambamo alielezasiasa kama mbinu ya kutafuta na kuteteautawala bila kujalimaadili au tofauti kati ya mema na mabaya.
Kitabu chake ambacho kimekuwa maarufu kinaitwa "Il Principe" (tamka: il prin-chi-pe) au "Mtawala". Humo alieleza masharti yautawala kwakiongozi wa kisiasa.
Sanamu ya Niccolo Machiavelli katika Jumba la Uffizi, Firenze.
Aliandika ya kwamba kuna vipindi vigumu katikamaisha yamataifa namadola ambapo anahitajika kiongozi wa kisiasa atakayeshika utawala na kutengeneza upya misingi ya dola. Katika utekelezaji wakazi hiyo anapaswa kushinda kwa namna yoyote akiondoa vizuizi na kila upinzani. Hatakiwi kubanwa na masharti walasheria za maadili.
Machiavelli aliandika ya kwamba ni afadhali kama mtawala anapendwa na kuhofiwa na wananchi kwa wakati uleule. Ila, kama anapaswa kuchagua kati ya kupendwa au kuhofiwa kwa sababu haiwezekani kuwa na pande zote mbili wakati mmoja, ni heri akihofiwa.
Pia ni ushauri wa Machiavelli kwamba matendo ya kinyama yatekelezwe haraka na vikali kwa sababu yatasahauliwa; lakini mema yatolewe polepole na kidogokidogo ili yakumbukwe kwamuda mrefu. Mtawala anatakiwa kuteteakanuni za mema mbele ya watu hata kama yeye mwenyewe atatenda kinyume chake lakini ikiwezekana kwasiri.
Haya yote yanatakiwamachoni pa Machiavelli kwa shabaha ya juu ambayo niheri yaumma. Utawala wa kiongozi mmoja uwe kipindi tu na shabaha iwejamhuri inayofuata sheria zake. Ila tu katika vipindi vya matatizo uongozi mkali unapaswa kuwepo.
Wight, Martin.Four Seminal Thinkers in International Theory: Machiavelli, Grotius, Kant, and Mazzini (2005), ch. 1online editionIlihifadhiwa 19 Juni 2009 kwenyeWayback Machine.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuNiccolo Machiavelli kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.