Nepal, rasmiJamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Nepal ninchi isiyo na pwani iliyoko katikaAsia ya Kusini, kati yaUchina kusini naIndia kaskazini-mashariki. Ina idadi ya wakazi takriban milioni 31, ikiwa ya 49 duniani kwa idadi ya watu. Mji mkuu na jiji kubwa zaidi niKathmandu. Lugha rasmi niKinepali. Nepal inajulikana kwa kuwa na sehemu kubwa yamilima ya Himalaya ikiwemoMlima Everest ambao ndio mkubwa zaidi duniani, urithi wake wakitamaduni nakidini, hasaUhindu naUbudha, na lenyehistoria tajiri yakifalme na mapambano yakidemokrasia.
Maeneo ya kijiografia ya Nepal yanayojulikana sana ni Himal, Pahad na Terai: Himal ni eneo lenye milima. Terai ni pahala palipo chini na Pahad ni milima isiyo natheluji.
Kwa kawaida nchi ya Nepal huwa namvua ya kutosha japo kunabaridi nyingi zakipupwe.
Misitu ya nchi hii imekuwa ikififia kutokana na ukataji holela wamiti.
Viongozi wa kwanza nchini Nepal walikuwa wanaKirati.Historia ya Nepal yaonyesha kwamba kulikuwa na kadri yahimaya 30 za wanaKirati walioongoza nchi hii.
Siasa
Kisiasa Nepal iko katika kipindi chamageuzi. Hadimwaka2006mfalme alitawala peke yake baada ya kuvunjabunge. Mwaka huo alilazimishwa kurudisha bunge, nalo lilitangaza ya kwamba mfalme hanamamlaka tena likamteua Mkuu wa nchi kwa muda. Tena kwamba bunge jipya litakalochaguliwa mnamoJuni2007 litaamua juu yakatiba mpya.
Utalii ndiouti wa mgongo wauchumi wa Nepal. Nchi hii hupendwa na watalii wanaopenda kuzuru na kuikwea milima yake kama mlima Everest, milima ya Himal na Pahad.
Mengine yanayowapendeza watalii ni kuwatazamandege wa nchi hii na kupaa juuangani kwa kutumiabaluni zilizo nahewa iliyopashwamoto.
Watalii pia hupenda kuzuru nchi hii kwa sababu ya dini ya Kibudha ambayo imejikita mizizi.
1. Nchi ina maeneo katikaAsia naUlaya. 2. Nchi ikoAsia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi zaUlaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Makala hii kuhusu maeneo yaAsia bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusuNepal kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.