Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Ndoa ya jinsia moja

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
     Nchi ambazo huruhusu harusi za jinsia moja     Nchi zinazotambua ndoa za wapenzi wa jinsia moja iliyofanywa mahali pengine     Nchi hizi huruhusu makubaliano yanayofanana na ndoa     Nchi hizi hazitambui makubaliano ya wapenzi wa jinsia moja

Ndoa za jinsia moja ni makubaliano kati yawanaume wawili auwanawake wawili ili kuishi pamoja kwa mfano wamume namke.

Ndoa ya namna hiyo ni halali katika nchi zaidi yaishiriniduniani. Nchi hizo (kwa mwaka wa2019, na kwa mpangilio wa muda wa idhini) ni:Uholanzi,Ubelgiji,Uhispania,Kanada,Afrika Kusini,Norwei,Uswidi,Ureno,Aisilandi,Ajentina,Denimaki,Brazil,Ufaransa,Uruguay,Nyuzilandi,Uingereza naWelisi,Uskoti,Luxemburg,Marekani,Eire,Grinilandi,Kolombia,Ufini,Visiwa vya Faroe,Malta,Ujerumani,Australia,Austria,Taiwan naEkuador.

Majimbo mengi hukoMexiko pia huruhusu ndoa yajinsiamoja. Majimbo yote katika Mexico lazima yatambue ndoa hizi.

Israeli inatambua ndoa zilizofanywa nje ya nchi.

Sheria itapaswa kubadilishwa hukoEire ya Kaskazini naKosta Rika. HukoPanama pia walisema watahalalisha ndoa ya jinsia moja.Mahakama ya Amerika Nzima ya Haki za Binadamu imeamua kuhalalisha ndoa ya jinsia moja. Uamuzi wake ni wa lazima kwa nchi zote zaAmerika ya Kilatini isipokuwa kwaVenezuela naKuba, lakini nchi zotembili zinajadili kuhalalishwa bila kujali.

Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu imeonyesha kwambakorti hiyo iko tayari kutangaza ndoa ya jinsia mojahaki za binadamu mara nchi za kutosha zitakapoihalalisha.

Pia kumekuwa na mazungumzo juu ya kuhalalisha ndoa kama hizo katika nchi zaAsia kamaUfilipino,Uthai,Kamboja,Nepali naJapani.Singapuri,Hong Kong naBeijing hutoa haki za kuishi kwa wanandoa wa jinsia moja wa kigeni, lakini haitoi ruhusa ya kuunda vyama kama hivyo kwaraia zao.

Nchi nyingine nyingi, hasa zaAfrika na zaKiislamu, hazikubali mahusiano ya namna hiyo kwa kuyaona ni kinyume chemaumbile yawatu natabia ya ndoa kuhusiana nauzazi. Hivyo wanapinga kwamba hii nihaki ya binadamu.

Kwa msingi huohuo nchi kadhaa zinaruhusu makubaliano yanayofanana na ndoa lakini hayaitwi "ndoa". Hizi (kwaherufi yaalfabeti) niAndorra,Aruba,Chile,Eire ya Kaskazini,Estonia,Hungaria,Italia,Kroatia,Kupro,Liechtenstein,San Marino,Slovenia,Ucheki,Ugiriki naUswisi.

Suala likoje

[hariri |hariri chanzo]

Tangumwaka2000idadi inayozidi kuongezeka ya nchi zimeanza kuruhusu ndoa kati ya watu wawili wajinsiamoja. Kumbe nchi nyingine zinapinga vikali jaribio hilo kama kinyume chadini nadesturi au hatamaumbile yenyewe.

Tabia zakingono kati yawanyama wa jinsia moja zimeonekana katikaspishi 500 hividuniani kote,[1][2] lakini wanaosema kuwaushoga ni kinyume cha maumbile wanamaanisha maumbile ya binadamu yanayotakiwa kuongozwa naakili nautashi, sisilika tu kama ilivyo kwaviumbehai wengine wote. Kwa mfano,ubakaji unafanywa na wanyama mbalimbali, lakini kwa binadamu haufai kabisa.

Takwimu zinaonyesha kwamba katikandoa za jinsia mojauaminifu wamoyoni na wamwilini ni mdogo kuliko katika ndoa za jinsiambili.[3] Pia "Idara ya Haki" ya Marekani imeripoti matukio ya ukatili mengi sana katika jozi za jinsia moja kuliko ya zile za jinsia mbili[4] kama ilivyowahi kuonyeshwa na utafiti waChuo Kikuu cha Michigan[5]

Uchunguzi mwingi umeonyesha kwamba wanaume waliofunga ndoa za jinsia moja wana kiwango cha talaka cha chini kidogo kikilinganishwa na kile cha watu waliofunga ndoa za jinsia mbili[6][7] na zile za wanawake wawili.[8][9]

Kiwango cha juu cha talaka kati ya wanawake kinapatana na takwimu zinazoonyesha kwamba kwa ujumla wanawake ndio wanaoanzisha talaka zilizo nyingi.[10][11]

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. Bagemihl, Bruce (1999).Biological Exuberance: Animal Homosexuality and Natural Diversity. St. Martin's Press.ISBN 978-0-312-25377-6.
  2. Harrold, Max (1999-02-16)."Biological Exuberance: Animal Homosexuality and Natural Diversity".The Advocate, reprinted in Highbeam Encyclopedia. Iliwekwa mnamo2007-09-10.
  3. Symons suggests that all men are innately disposed to want sexual variation and that the difference between heterosexual and homosexual men is that homosexual men can find willing partners more often for casual sex, and thus satisfy this innate desire for sexual variety. Harris, C. R. (2002). "Sexual and romantic jealousy in heterosexual and homosexual adults". Psychological Science. 13 (1): 7–12. doi:10.1111/1467-9280.00402.PMID 11892782.
  4. "Nakala iliyohifadhiwa"(PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo(PDF) mnamo 2022-07-31. Iliwekwa mnamo2022-07-30.
  5. https://www.lifesitenews.com/news/study-almost-half-of-gay-men-abused-by-their-partners/
  6. Marian Jones (1 Mei 1997)."Lessons from a Gay Marriage: Despite stereotypes of gay relationships as short-lived, gay unions highlight the keys to success".Psychology Today. Iliwekwa mnamo20 Aprili 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Andersson, Gunnar (Februari 2006)."The Demographics of Same-Sex 'Marriages' in Norway and Sweden"(PDF).Demography.43 (1): 79–98.doi:10.1353/dem.2006.0001. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo(PDF) mnamo 2009-03-25. Iliwekwa mnamo2019-07-24.{{cite journal}}:Unknown parameter|dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. EL."Marital Bliss? Gender Gaps..."Gender Across Borders. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2015-12-27. Iliwekwa mnamo26 Desemba 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. https://www.lifesitenews.com/blogs/skyrocketing-lesbian-divorce-rates-show-failure-of-same-sex-couples-imitating-marriage
  10. In the Netherlands of the 580 lesbian couples who were married in 2005, 30% were divorced ten years later compared to 18% for heterosexual couples and 15% for gay male couples.Janene Pieters (1 Machi 2016)."Marriages Between Women Most Likely To End In Divorce".NL Times. Iliwekwa mnamo17 Mei 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. Marian Jones (1 Mei 1997)."Lessons from a Gay Marriage: Despite stereotypes of gay relationships as short-lived, gay unions highlight the keys to success".Psychology Today. Iliwekwa mnamo20 Aprili 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuNdoa ya jinsia moja kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuNdoa ya jinsia moja kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Ndoa_ya_jinsia_moja&oldid=1425140"
Jamii:
Jamii zilizofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp