Nabii Mika, ambaye jina lake laKiebraniaמיכה linamaanisha "Nani kamaMungu?", alifanyakazi yaunabii wakati mmoja naIsaya (miaka740-700 hiviK.K.), chini yaYotamu,Ahazi naHezekia,wafalmewa Yuda.
Tangu kale anaheshimiwa kamamtakatifu, hasatarehe21 Desemba[1] na14 Agosti, lakini pia14 Januari,18 Januari na31 Julai[2].
Ujumbe wake unajulikana kupitiakitabu chenyejina lake katikagombo laManabii Wadogo (Kitabu cha Mika)
Humo tunasoma kwamba yeye, kama vile Isaya, aliteteahaki za wanyonge (2:1-11), alipingaibada zamiungu nadhuluma pamoja na kutabiriadhabu.
Lakini hasa alilitabiriataifa teule juu yaMasiya, kwamba mfalme aliyeahidiwa tangu kale atazaliwaBethlehemu (5:1-3), tunavyosoma katikaInjili ya Mathayo kuhusuuzazi waYesu Kristo, na kwamba atachungaIsraeli kwa nguvu yaBwana[3].
![]() | Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuNabii Mika kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari. |