Waisraeli walielekeadini za kandokando kwa sababu zilikuwa zinaahidi kufanikishamaombi yao kwaibada zahakika, wakatiMungu anahiari ya kupokea au kukataasadaka zao. Waisraeli walijaribu kufuata pande zote mbili kwa pamoja, ila Mungu hakuweza kukubali, kwa kuwa ni peke yake tu.Imani yao iliyumba hasa wakatimfalme Ahabu alipotawala Kaskazini (869-850 hiviKK) ambapoYezebeli,mke wake, alifanyajuhudi kubwa za kuikomesha kabisa imani yao kwa YHWH ili wamuabudu Baali, mungu mkuu wa kwao aliyehusika namvua, kufuatana na sanamu mbili zilizotengenezwa namfalme Yeroboamu I zikiwa na sura ileile ya Baali (fahali wa dhahabu). Mezani pamalkia huyo walikuwa wanalishwa manabii wa uongo 850huyo walikuwa wanalishwa manabii wa uongo 850, kumbe manabii wa Bwana waliuawa karibu wote.
HapoMungu akamtuma Eliya waTishbi (1Fal 17-18) ambayejina lake lina maana ya kwamba, “Mungu wangu ni YHWH” na linajumlishakazi yake ya kutetea kwaari zote imani ya kweli hata akaiokoa. Ili kuondoautata wa kuabudu pande mbili, Eliya kwanza alizuia mvua isinyeshe nchini miaka mitatu na nusu, ibada kwa Baali zisifanikiwe hata kidogo, halafu akashindana na manabii haohadhara ya Israeli yote juu yamlima Karmeli. Tofauti nambinu za manabii 450 wa Baali, waliofikia kujichanja na kutokadamu ili kuvutamoto kutokambinguni wasifaulu, Eliya aliomba tu kwaunyofu kwamba Mungu ajitokeze ili kugeuza mioyo ya watu wake wamrudie. Kwa kuteremsha moto toka mbinguni juu ya sadaka yake YHWH alithibitisha kuwa ndiye Mungu pekee na kuwa anaendelea kuwaokoa watu wake. Baada ya Eliya kuwachinja wote aliruhusu mvua inyeshe tena. Ndiyo sababu anasifika kwa nguvu ya sala yake (Yak 5:17-18).
Hasa ni kwamba, baada ya kukimbiahasira ya Yezebeli aliyemuapia atamuua kabla yakesho yake, akisalipangoni juu yamlima Sinai kamaMusa mwanzoni mwa agano la Israeli naBwana, alijaliwa kutokewa na kuagizwa upya na Mungu katika sauti ndogo ya upepo mtulivu akamilishe kazi yake hasa kwa kuwafanyaElisha nabii naYehu mfalme (1Fal 19:1-18). Hata katikaYesu kugeuka sura mlimani akatokea pamoja na Musa ili wamshuhudie kama wawakilishi waTorati naManabii (Mk 9:2-13).
Kwa jinsi alivyofanya kazi kwaari, na kwa kupalizwa juu ya gari la moto (2Fal 2:1-18) akalinganishwa na moto (YbS 48:1-11) akatabiriwa atarudi kabla ya siku ya Bwana (Mal 3:23-24).
"Ee Bwana, Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Israeli,na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli,na ya kuwa mimi ni mtumishi wako,na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako.Unisikie, Ee Bwana, unisikie, ili watu hawa wajueya kuwa wewe, Bwana, ndiwe Mungu,na ya kuwa wewe umewageuza moyo wakurudie". (1Fal 18:36-37)
"Yatosha! Sasa, Ee Bwana, uiondoe roho yangu;kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu". (1Fal 19:4)
Kati ya wanafunzi wake (walioitwawana wa manabii) kazi yake kwa miaka zaidi ya 50 iliyeendelezwa hasa nanabii Elisha, ambaye anasifika pia kwa miujiza yake (YbS 48:12-16) na pamoja na mwalimu wake amechukuliwa naYesu Kristo kama mfano waunabii wake utakaowaokoa mataifa baada ya Israeli kumkataa (Lk 4:24-27). Elisha alijihusisha sana nasiasa akaombwashauri na wafalme mbalimbali hata wanchi za nje. Kwa kumpakamafuta Yehu alianzishamapinduzi dhidi yaukoo wa Ahabu na kukomeshaupotoshaji wake wa imani. Mapinduzi hayo yakaeneakusini kwa kumuuaAtalia, binti wa Yezebeli, aliyetawala miaka saba kisha kuua watu wote wa ukoo waDaudi (mtotoYoashi tu alinusurika).
John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 204
Pd. Leandry Kimario,O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 171
Bialik, H. N. and Y. H Ravnitzky. eds.The Book of Legends: Sefer Ha-Aggadah. New York: Schocken Books, 1992.ISBN 0-8052-4113-2
Ginzberg, Lewis.Legends of the Bible. Philadelphia: Jewish Publication Society of America, 1956.
Schwartz, Howard.Tree of Souls: The Mythology of Judaism. Oxford: Oxford University Press, 2004.ISBN 0-19-508679-1
Wolfson, Ron and Joel L. Grishaver.Passover: The family Guide to Spiritual Celebration. Woodstock, VT: Jewish Lights Publishing, 2003.ISBN 1-58023-174-8
Sydelle, Pearl.Elijah's Tears: Stories for the Jewish Holidays. New York: Holt Publishing, 1996.ISBN 0-8050-4627-5
Thaler, Mike.Elijah, Prophet Sharing: and Other Bible Stories to Tickle Your Soul. Colorado Springs, CO: Faith Kids Publishing, 2000.ISBN 0-7814-3512-9
Scheck, Joann.The Water That Caught On Fire. St. Louis, Missouri: Concordia Publishing House: ARCH Books, 1969. (59-1159)
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuNabii Eliya kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.