NASA ni kifupi chaKiingereza cha "National Aeronautics and Space Administration" (Mamlaka ya Taifa ya Uanahewa na Ange-nje). Mamlaka hii ilianzishwa 1958. Wajibu wake ni kusimamia miradi ya serikali yaMarekani ya kuendesha utafiti na uchunguzi wa anga. NASA inasimamia utengenezaji wa roketi za kurusha vyombo vya angani na utengenezaji wa vyombo vya angani vyenyewe.
Roketi iliyorusha "Freedom 7" na Alan Shepard Jr.angani tar. 5.5.1961
Miradi ya NASA ilianzishwa kutokana naMshtuko wa Sputnik yaani baada yaWarusi kushtusha dunia kwa kupeleka vyombo vya angani vya kwanza katika mradi wao waSputnik. Uliofuatiwa na mradi wa "Vostok" ambao tarehe12 Aprili1961 ulimfikishaYuri Gagarin angani akiwa mtu wa kwanza kwenda angani.
Mradi wa kwanza wa NASA ulikuwaMradi wa Mercury uliotakiwa kuonyesha ya kwamba wanaanga wanaweza kukaa angani kwa muda fulani. Alan B. Shepard Jr. alikuwa Mmarekani wa kwanza angani kwa muda wa dakika 15; John Glenn alikuwa Mmarekani wa kwanza wa kuzunguka dunia tarehe20 Februari1962 kwa chombo cha angani "Friendship 7".
Mradi huo ulifuatiwa naMradi wa Gemini kuanzia mwaka 1965 ulionyesha ya kwamba watu wanaweza kukaa angani kwa muda wa siku kadhaa hata kutekeleza shughuli fulani. Gemini iliandaaMradi wa Apollo uliopeleka watu wa kwanzamwezini. Chombo cha angani "Apollo 11" kilifikisha wanaangaNeil Armstrong naBuzz Aldrin kwenye uso wa mwezi tarehe20 Julai1969 na kuwarudisha dunia tena.
Tangu mwanzo ule kuna miradi mingi iliyofuata.
Buzz Aldrin akitembea kwenye uso wa mwezi wakati wa safari ya Apollo 11.