Mzungu (wingi:wazungu) ni neno laKiswahili kumtaja mtu anayeonekana ametokaUlaya. Mara nyingi, mtu ambaye amechukua utamaduni wa Kiulaya huitwa "Mzungu" hata asipokuwa na nasaba ya Kiulaya. Kwa hivyo, "Mzungu" ina fasili mbalimabli.
Ni neno ambalo zaidi linalengarangi ya mtu na kumtofautisha yule anayetajwa naMwafrika,Mwarabu,Mhindi auMchina.
Si neno kamili sana kwa sababu watu wanaoitwa Wazungu wanaweza kutokea kila sehemu yadunia;Wamarekani weupe huitwa Wazungu na piamakaburu kutokaAfrika Kusini,Wakenya weupe na piaWaaustralia. Vilevile mtu kutoka nchi zaUlaya ya Kusini kamaHispania auUgiriki anaweza kusababisha wasiwasi kama yeye ni Mzungu au Mwarabu kwa sababu wengi wao hufanana na watu waAfrika ya Kaskazini.
Ikitumiwa kwa maana ya "watu wa Ulaya" inaeleweka kwa jumla isipokuwa siku hizi nchi za Ulaya hujaa watu ambao wenyewe au mababu wao walihamia huko kutoka pande nyingi za dunia jinsi inavyoonekana kwenye nyuso yao.
Kiasili neno lilijitokeza wakati ambako watu waliweza kuamini ya kwamba kila sehemu ya dunia ilikuwa na rangi yake. Kwa namna hiyo inafanana na maneno katikalugha nyingine kwa mfano "negroe/negre/Neger" katika lugha za Ulaya kwa watu wanaoonekana kama wenye asili ya Kiafrika. Hainadharau ndani yake kama neno laKiarabu "abdi" linalotaja watu weusi pamoja nawatumwa.
Neno "Kizungu" linatumiwa mara nyingi kwa maana ya lugha yaKiingereza, lakini wakati waukoloni waUjerumani katikaTanzania bara ("Afrika ya Mashariki ya Kijerumani") lilitaja piaKijerumani[1].
Asili ya neno haijulikani kikamilifu. Inaonekana kuna uhusiano na neno mzungu / mizungu lisilo kawaida tena katikaKiswahili cha kisasa lakini limetunzwa katikakamusi za Kiswahili zilizokusanya maneno yake mnamo mwaka1900. Lilimaanisha mambo mbalimbali kama vile: 1) kitu chaajabu au cha kushangaza, 2)mbinu ya kujiondoa katikatatizo, 3) aina yamuhogo, 4)silika auakili yawanyama.[2]
Waswahili waliwahi kutumia neno "mzungu" kwa "akili" na pia kwa mafundisho ya "unyago" yaliyoitwa "kufundishwa mizungu".[3]. Kama asili ya "Wazungu" iko hapa iliweza kumaanisha "watu wa ajabu, wasio kawaida, wenye mbinu nyingi" au "wageni walio tofauti sana".
Wengine wamehisi kwautani ya kwamba kunauhusiano nakitenzi "kuzunguka" na "mzungu" ilitaka kutajatabia yawapelelezi,wamisionari nawafanyabiashara wa kwanza kutoka Ulaya ambao hawakukaamahali pamoja bali walizungukazunguka kote Afrika.