Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Myanmar

Majiranukta:22°N96°E /22°N 96°E /22; 96
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Pyidaunzu Thanmăda Myăma Nainngandaw

Jamhuri ya Muungano wa Myanmar
Bendera ya MyanmarNembo ya Myanmar
BenderaNembo
Kaulimbiu ya taifa:
Wimbo wa taifa:Kaba Ma Kyei
Lokeshen ya Myanmar
Mji mkuuNaypyidaw1
19°45 N 96°12 E
Mji mkubwa nchiniYangon
Lugha rasmiKiburma
Serikali
Win Myint
Aung San Suu Kyi
Uhuru
Tarehe
4 Januari1948
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
676,578 km² (ya 40)
3.06%
Idadi ya watu
 - [[]] kadirio
 -2014 sensa
 - Msongamano wa watu
 
(ya 25)
51,486,253
76/km² (ya 125)
FedhaKyat ya Myanmar (K) (mmK)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
MMT (UTC+6:30)
{{{time_zone_DST}}} (UTC{{{utc_offset_DST}}})
Intaneti TLD.mm
Kodi ya simu+95

-

1Serikali kadhaa hutambua Yangon kama mji mkuu.


Myanmar, rasmi kamaJamhuri ya Muungano wa Myanmar, pia hujulikana kamaBurma, ni nchi iliyokoAsia ya Kusini-Mashariki. Inapakana naBangladesh naIndia magharibi,China kaskazini,Laos naUthai mashariki, naBahari ya Andamani pamoja naGhuba ya Bengali kusini. Ina idadi ya watu takriban milioni 55, ikiifanya kuwa ya 26 duniani kwa idadi ya watu. Mji mkuu niNaypyidaw, ingawa jiji kubwa zaidi na kitovu cha kibiashara niYangon (Rangoon). Lugha rasmi niKiburma (Burmese), na nchi imegawanyika katika mikoa na majimbo 21. Inajulikana kwa hekalu lake kuu la Shwedagon, historia ndefu ya kifalme, mitaa ya Yangon yenye majengo ya kikoloni, na vilevile changamoto zake za kijamii na kisiasa katika karne ya 21.

Jiografia

[hariri |hariri chanzo]

Kaskazini mwa nchi kunamilima mingi.Safu tatu zaRakhine Yoma,Bago Yoma naNyanda za Juu za Shan zimeanza katikaHimalaya na kuelekea kusini. Milima yaHengduan Shan iko mpakani kwa China. Mlima mkubwa niHkakabo Razi kwenye jimbo la Kachin wenyekimo cha mita 5,881.

Mito mitatu mikubwa ya Myanmar inavuka kati ya safu za milima; niː

Mto Ayeyarwady ni mto mkubwa wa Myanmar wenye urefu wa km 2,170.Bonde lake ni larutuba na lina wakazi wengi.

Karibunusu ya nchi imefunikwa namisitu.

Miji mikubkwa

[hariri |hariri chanzo]
Nafasi mwaka 2006MjiSensa ya 1983Kadirio kwa 2006Dola / Mkoa
1.Yangon (Rangoon)2,513,0234,572,948Mkoa wa Yangon
2.Mandalay532,9491,237,028Mkoa wa Mandalay
3.Naypyidaw (Nay Pyi Taw) *0924,608Eneo la Kitaifa Naypyidaw
4.Mawlamyaing219,961451,011Dola la Mon
5.Bago150,528248,899Mkoa wa Bago
6.Pathein144,096241,624Mkoa wa Ayeyarwady
7.Monywa106,843185,783Mkoa wa Sagaing
8.Meiktila96,492181,744Mkoa wa Mandalay
9.Sittwe107,621181,172Dola la Rakhine
10.Mergui88,600177,961Mkoa wa Tanintharyi
11.Taunggyi108,231162,396Dola la Shan

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Tangukarne ya 9BK nchi iliona falme mbalimbali zilizotawala kutoka mji mkuu waPagan.

Katikakarne ya 19Uingereza ulianza kujishughulisha na habari za Burma (Myanmar) baada ya kutawala maeneo jirani ya Uhindi. Kwavita tatu kati ya miaka1826 na1885 Uingereza ulieneza utawala wake.

Burma ilikuwa sehemu yaUhindi wa Kiingereza tangu 1885.

Mwaka1937 Waingereza walianza kutawala Burma kamakoloni la pekee.

Wakati waVita Kuu ya Pili ya DuniaJapan ilitwaa karibu nchi yote.

Baada ya vita Burma ikapatauhuru wake tarehe4 Januari1948.

Serikali iliyochaguliwakidemokrasiailipinduliwa na jeshi mwaka1962.

Mtawala mpya hadi mwaka1988 alikuwajeneraliNe Win aliyetangazasiasa ya "Ujamaa wa Kiburma".Upinzani ulikandamizwa vikali mara kadhaa.

Nchi ilionaharakati kwa ajili ya demokrasia na dhidi yaudikteta mwaka 1988; hapo Ne Win alijiuzulu.

Baada yamaandamano yaliyokandamizwa mara kadhaa, JeneraliSaw Maung alichukua utawala kwa nguvu ya kijeshi.

Uchaguzi huru wa mwaka1989 uliletaushindi wachama cha NLD, chini yaAung San Suu Kyi, lakini kamati ya kijeshi ilikataa kukabidhimadaraka.

Burma ilibadilishiwa jina kuitwa "Myanmar" ikaendelea kutawaliwa naserikali ya kijeshi hadi mwaka2011. Upinzani haukuruhusiwa.

Utawala

[hariri |hariri chanzo]

Myanmar imegawiwa kwa kusudi la utawala katika madola 7 namikoa 7. "Madola" ni maeneo yanayokaliwa na jumuiya na makabila ambayo ni tofauti na kundi kubwa la taifa linaloitwaBamar. Maeneo ya Bamar huitwa mikoa.

Majimbo ya Myanmar

Madola ya jumuiya ndogo yapo zaidi karibu na mipaka ya nchi. Kuanzia kusini-magharibi ni haya yafuatayo:

Halafu kuna mikoa 7:

Mazingira yamji mkuuNaypyidaw ni eneo la kitaifa la Naypyidaw.

Madola na mikoa imegawiwa katikawilaya,tarafa,kata navijiji.

Watu

[hariri |hariri chanzo]

Myanmar ni nchi ya makabila mengi (135 yametambulika rasmi) nalugha nyingi (angaliaorodha ya lugha za Myanmar). Kundi kubwa (68%) niWaburma wenye asili katika milima yaTibet walikotokea mababu wao miaka 1000 hivi iliyopita.

Lugha kubwa niKiburma, ambacho ndicholugha rasmi.

Wakazi walio wengi (80%) hufuatadini yaUbuddha, hasa yamadhehebu yaTheravada.Wakristo ni 7%, wafuasi wadini za jadi ni 6%,Waislamu ni 4%,Wahindu ni 2%.

Picha

[hariri |hariri chanzo]

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Taarifa za jumla
Uchumi
Kilimo
Biashara

22°N96°E /22°N 96°E /22; 96


Nchi na maeneo yaAsia

Afghanistan |Armenia2 |Azerbaijan |Bahrain |Bangladesh |Bhutan |Brunei |China |Falme za Kiarabu |Georgia2 |Hong Kong3 |Indonesia |Iran |Iraq |Israel |Jamhuri ya China (Taiwan) |Japani |Kamboja |Kazakhstan |Kirgizia |Korea Kaskazini |Korea Kusini |Kupro2 |Kuwait |Laos |Lebanoni |Macau3 |Malaysia |Maldivi |Mongolia |Myanmar |Nepal |Omani |Pakistan |Palestina |Qatar |Saudia |Singapuri |Sri Lanka |Syria |Tajikistan |Timor ya Mashariki |Turkmenistan |Ufilipino |Uhindi |Urusi1 |Uthai |Uturuki1 |Uzbekistan |Vietnam |Yemen |Yordani

1. Nchi ina maeneo katikaAsia naUlaya. 2. Nchi ikoAsia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi zaUlaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Makala hii kuhusu maeneo yaAsia bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuMyanmar kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Myanmar&oldid=1467603"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp