Awamu za Mwezi - Mwezi mwandamo ni na. 1 (Nuru ya Jua kutoka kushoto)Awamu za mwezi kuanziamwezi mwandamo (1) kupitiahilali (2), robo ya kwanza, nusu mwezi, robo ya tatu,mwezi mpevu (5) hadi mwezi mwandamo tena
Mwezi mwandamo (kwaKiing.New Moon) ni awamu yaMwezi ambapo hauonekani kwamacho. Awamu hiyo inatokea kila baada yasiku 291/2.
Katika awamu hiyo Mwezi uko kati yaDunia naJua. Hivyo ni nusu ya Mwezi isiyoonekana kutoka Duniani ndiyo inayopokeanuru ya Jua lakini upande ambao tunatazama ukokivulini[1].
Hali halisi upande unaotazama Dunia hauko gizani kabisa kwa sababu unapokea kiasi cha nuru inayoakisiwa kutoka uso wa Dunia. Lakini wakati wa mchana nuru ya Jua ni kali zaidi hivyo hatuoni Mwezi.
Ilhali Mwezi uko kati ya Jua na Dunia, kuna hali ya pekee. Kama Mwezi unapita kamili mstari uliopo baina ya Jua na Dunia, unafunika Jua kwamuda mfupi. Kwa njia hiyo kivuli cha Mwezi kinapita kwenye uso wa Dunia. Watu waliopo katika eneo la kivuli chake wanaonakupatwa kwa Jua[2].