Mwandiko wa Kichina ni jumla yaalama zinazotumiwa kuandikalugha zaKichina.Mwandiko huo hutumia alama moja kwaneno lote kwa hiyo kila mtu anaelewa mwandiko hata akisoma na kutamka tofauti katikalahaja mbalimbali.
Kichina huandikwa kwa alama zinazomaanisha neno moja. Alama hizo hazimaanishiherufi fulani walasilabi jinsi ilivyo katika miandiko mingine. Kwa hiyo watu wawili wanaweza kusoma alama hizohizo na kutamka tofauti wakitumia lahaja tofauti au hata aina za Kichina tofauti; hata wasipoelewana wakati wa kuongea, wote wanaelewa maana ya alama hata wakitamka maneno tofauti.
Maneno mengi ya Kichina yana silabi moja tu.Kamusi kubwa ya lugha ina alama zaidi ya 40,000- Wachina wasomi wenyeelimu nzuri hujua takriban alama 6,000 hadi 7,000.Gazeti la kawaida hutumia alama 3,000.Serikali inasema mtu ajua kuandika na kusoma kama ameshika angalau alama 2,000.
Chanzo cha alama kwenye mwandiko wa Kichina nipicha. Vyanzo hivyo vinafanana namitindo iliyotumiwa kwinginekoduniani kamaBabeli. Lakini ilhali katika mifumo mingine picha zilirahisishwa na kutumiwa kwa silabi ausauti tu na kuwa herufi, China ilibaki na picha moja kwa neno moja ilhali picha zilirahisishwa na kuwa alama kwa urahisi wa kuandika haraka.
Tangu maungano ya kwanza ya Chinaserikali kuu iliratibuusanifishaji wa alama. Alama jinsi zilivyosanifishwa miaka 1800 hutumiwa hadi leo hii.
Mabadiliko ya alama kwa "farasi" katika mwandiko wa Kichina tangu kale hadi leo
Katikakarne ya 20 kulikuwa namajadiliano nchini China kurahisisha namna ya kuandika maanaWachina wengi hawakuweza kuandika na kusoma au walijua alama chache tu. Wengine walipendekeza kuachana kabisa na alama za kidesturi na badala yake kuhamia alfabeti ya Kilatini. Wengine waliona itasaidia kupunguzaidadi yamistari nanukta katika alama zinazohitajika mara kwa mara.
Baada ya mapinduzi ya 1949 serikali yaKikomunisti ilitangaza orodha ya alama zilizorahisishwa. Hizo zinafundishwashuleni lakini zinatumiwa pamoja na alama za zamani ambazo ni tata zaidi, hasa kwa ajili yaistilahi ambazo hazitumiwi mara kwa mara.
NchiniJapani alama nyingi za Kichina zinatumiwa pamoja na alama za ziada kwa kuandikaKijapani. Pia Japani serikali ilifanya mabadiliko katika mwonekano wa alama kwa shabaha za kuzirahisisha ili zishikwe haraka zaidi nawanafunzi.
Hapo chini mifano kadhaa ya alama zinazotumiwa upande wa Kichina na Kijapani, pamoja na mabadiliko yao kwa lengo la kuzirahisisha:
Ulinganishi wa Alama Sanifu (za Zamani), Alama Sanifu Zilizorahisihwa na Alama sanifu za Kijapani za Kisasa
Kichina
Kijapani
Maana yake
Alama Sanifu za Kichina (za zamani)
Alama za Kichina zilizorahisishwa
Alama zilizorahisishwa China Bara tu, lakini siyo Japani
電
电
電
umeme
買
买
買
kununua
車
车
車
gari
紅
红
紅
nyekundu
無
无
無
hamna, hakuna kitu
東
东
東
mashariki
馬
马
馬
farasi
風
风
風
upepo
愛
爱
愛
upendo
時
时
時
wakati
鳥
鸟
鳥
ndege
島
岛
島
kisiwa
語
语
語
lugha, neno
頭
头
頭
kichwa
魚
鱼
魚
samaki
園
园
園
bustani
長
长
長
ndefu, kukua
紙
纸
紙
karatasi
書
书
書
kitabu, hati
見
见
見
angalia, tazama
Alama zilizorahisishwa katika Japani lakini si China Bara
假
假
仮
bandia, kukopa
佛
佛
仏
Buddha
德
德
徳
maadili
拜
拜
拝
kusali, kuabudu
黑
黑
黒
nyeusi
冰
冰
氷
barafu
兔
兔
兎
sungura
每
每
毎
kila
壤
壤
壌
udongo
步
步
歩
hatua
惠
惠
恵
neema
Alama zilizorahisishwa tofauti katika China na Japani
圓
圆
円
duara
聽
听
聴
sikia
實
实
実
halisi
證
证
証
uthibitisho
賣
卖
売
kuuza
龜
龟
亀
kobe
藝
艺
芸
sanaa
戰
战
戦
vita, kupigana
繪
绘
絵
taswira, picha
鐵
铁
鉄
chuma
團
团
団
kundi, kikosi
轉
转
転
Kugeuka
惡
恶
悪
ubaya, chuki
豐
丰
豊
tele, kwa wingi
腦
脑
脳
ubongo
壓
压
圧
shinikizo
雞/鷄
鸡
鶏
kuku
價
价
価
bei
樂
乐
楽
muziki
氣
气
気
hewa
廳
厅
庁
ukumbi, ofisi
勞
劳
労
kazi
劍
剑
剣
upanga
歲
岁
歳
umri, miaka
燒
烧
焼
kuwaka
贊
赞
賛
kusifu
兩
两
両
mbili
譯
译
訳
tafsiri
觀
观
観
kuangalia, kutazama
齒
齿
歯
meno
藥
药
薬
dawa
讀
读
読
kusoma
顏
颜
顔
uso
Alama zilizorahisishwa karibu sawa China bara na Japani
Chinese Text Project Dictionary Comprehensive character dictionary including data for all Chinese characters in Unicode, and exemplary usage from early Chinese texts.
Unihan Database: Chinese, Japanese, and Korean references, readings, and meanings for all the Chinese and Chinese-derived characters in theUnicode character set
Daoulagad Han– Mobile OCR hanzi dictionary, OCR interface to the UniHan database