Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Mwanaanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwanaanga Piers Sellers nje ya chombo chaspace shuttle tarehe 12 Juni 2006.

Mwanaanga nimtu anayerushwa katikaanga-nje yaanianga lililo nje yaangahewa yadunia.Majina mengine yaliyokuwa kawaida ni "kosmonauti" (kwaKirusi: космонавт) kwa wanaangaWarusi na "astronauti" (kwaKiingereza astronaut) kwa wanaanga kutokaMarekani.Wachina wametumianeno "taikonauti".

Mwanaanga wa kwanza katikahistoria yabinadamu alikuwa MrusiYuri Gagarin kutokaUmoja wa Kisovyeti aliyerushwatarehe12 Aprili1961 kwachombo cha anganiVostok akizunguka dunia yote maramoja katikamuda wadakika 108.

Alifuatwa tarehe5 Mei 1961 naAlan Shepard kutokaMarekani aliyetumia chombo cha angani chaMercury .

Mwanamke wa kwanza angani alikuwa MrusiValentina Tereshkova mwaka1963.

Wanaanga wa kwanza waliofika kwenye uso waMwezi walikuwa WamarekaniNeil Armstrong naBuzz Aldrin tarehe20 Julai1969.

HadiMachi2008 jumla ya watu 477 kutoka nchi 39 walifika kwenye kimo chakilomita 100 juu ya uso wa dunia ambacho ni kimo ambako anga-nje linaanza kulingana na maelezo yaShirikisho la Kimataifa kwa Usafiri wa Angani (Fédération Aéronautique Internationale (FAI)).

Kati ya hawa ni 24 waliofika mbali kuliko kilomita 2,000 juu ya uso wa dunia hadi njia ya mwezi kwenye anga.

Mwanaanga aliyekaamuda mrefu angani alkuwa MrusiSergei Krikalyov aliyefika angani marasita akakaa jumla yasiku 803,saa 9 nadakika 39 kwenye anga-nje.

Baina ya miaka2001 hadi2009 watusaba walifika kwenye anga-nje kamawatalii yaani wageni waliolipia nafasi ya kusafiri pamoja na wanaanga hadiKituo cha Anga cha Kimataifa (ISS) walipokaa kwawiki moja. Walilipa zaidi yadolarmilioni 20. Mmojawao alikuwaMark Shuttleworth waAfrika Kusini.

Picha za wanaanga

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo yasayansi bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuMwanaanga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Mwanaanga&oldid=1301815"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp