Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Afrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutokaMwafrika)
Afrika duniani.
Afrika kutoka kwenyeMwezi (Ocktoba 2015)
Uwiano kati ya Afrika, Asia na Amerika.

Afrika nibara la piliduniani kwa ukubwa, likiwa na eneo lakilometa za mraba zipatazo 30,370,000 na kwaidadi ya wakazi, hao wakiwa 1,225,080,510 (mwaka2016).Asia ndiyo bara kubwa pekee zaidi ya Afrika.

Jina

Afrika kutokasatelaiti.

Neno "Afrika" limetokana nalugha yaKilatini yaRoma ya Kale.[1][2] kwajina hiloWaroma wa Kale walitaja eneo katikaTunisia ya leo, hawakumaanisha bara lote.

Inasemekanaasili yake nikabila la "Afrig" lililoishi sehemu zile,[3]lakini kuna pia maelezo mengine tofautitofauti.

Wakati huoWagiriki wa Kale walitumia zaidi jina laLibya kwa ajili ya nchikusini kwaBahari ya Mediteranea, upande wa magharibi wa Misri.

Maeneo ya ndani kuelekea kusini mara nyingi yaliitwa kwa jina la "Ethiopia" linalomaanisha nchi ya watu weusiweusi (kwaKigiriki "aithiops": aliyechomwa najua).

Katikaramani za kale kutokaUlaya maneno yote matatu ya "Afrika", "Lybia" na "Ethiopia" yanapatikana yakitumika kama jina la bara zima. Jina la "Afrika" limekuwa la kawaida kuanziakarne ya 16BK.

Jiografia

Afrika imezungukwa na bahari karibu pande zote. Kuna kiungo chembamba cha nchi kavu upande wakaskazinimashariki na bara la Asia kwenyerasi ya Sinai[4].

Upande wa kaskazini ikoBahari ya Mediteranea, upande wa mashariki kunaBahari Hindi pamoja naBahari ya Shamu na upande wa magharibi ikoBahari Atlantiki.

Kunakisiwa kikubwa chaMadagaska nafunguvisiwa mbalimbali.

Barani kunanchi huru 54 zinazotambuliwa naUmoja wa Mataifa, maeneo 9 yenye hali ya pekee namadola mawili ambayo yanajitawala bila kutambuliwa kimataifa.

Kunaumbali wakilomita 8,000 kutokaRas ben Sakka nchiniTunisia (37°21' N, sehemu ya kaskazini kabisa) hadi rasi yaCape Agulhas nchiniAfrika Kusini (34°51'15" S, sehemu ya kusini kabisa)[5].

Umbali ni km 7,400 kutoka upande wa magharibi (rasi yaCape Verde, 17°33'22" W) hadi mashariki (Ras Hafun nchiniSomalia, 51°27'52" E)[6].

Pwani yote ya Afrika inaurefu wa kilomita 26,000.

Nchi kubwa ya Afrika niAlgeria na nchi ndogo ni funguvisiwa laShelisheli katika Bahari Hindi.[7] Nchi ndogo Afrika bara niGambia.

Kijiolojia Afrika iko kwenyebamba la Afrika. Lilebamba la gandunia la Afrika linaenea mbali zaidi kuliko maeneo tunayotazama kuwa Afrikakijiografia, ni pamoja na maeneo chini ya bahari linapopakana namabamba ya Ulaya-Asia,Uarabuni,Uhindi naAustralia,Antaktika,Amerika ya Kusini naKaskazini. Upande wa mashariki wa bamba la Afrika kunaufa unaozidi kupanuka ikielekea kujitenga kutoka Afrika kamabamba la Somalia.

Tabianchi

Uoto barani Afrika

Tabianchi ya Afrika ni pana, kuanzia kanda zatropiki hadi kufikia maeneo yanusu-aktiki (baridi) kwenye ncha zamilima mirefu.

Nusu ya kaskazini ya bara nijangwa au angalauyabisi. Sehemu za kati na za kusini zina maeneo yasavanna na kanda zamsitu wa mvua.

Afrika ni bara lenyejoto kuliko mabara yote na asilimia 60 za uso wake ni maeneo yabisi aujangwa.[8]

Nchi za Afrika

Aljeria
Togo
Benin
Guinea ya Ikweta
Chadi
Misri
Uhabeshi
Eritrea
Cabo*
Verde
Libya
Mali
Ghana
Kodivaa
Burkina
Faso
Mauritania
Moroko
Sao Tome na Principe*
Nijeri
Gabon
Naijeria
Kongo
Somalia
Afrika Kusini
Namibia
Sudan
Tunisia
Sahara
ya Magharibi
Senegal
Gambia
Guinea
Bisau
Guinea
Liberia
Madagaska
Jamhuri ya
Afrika ya Kati
Kenya
Uganda
Tanzania
Burundi
Rwanda
Sudan
Kusini
Angola
Saint Helena (UK)*
Kamerun
Sierra
Leone
Lesoto
Zambia
Zimbabwe
Botswana
Morisi*
Réunion*
*Komori
Shelisheli
Jamhuri ya
Kidemokrasia
ya Kongo
Eswatini
Msumbiji
Malawi
Jibuti
Bahari ya
Atlantiki
Bahari ya
Atlantiki
Bahari
ya Hindi
Mlango wa bahari wa Gibraltar
Bahari ya Mediteranea
Bahari
ya Shamu


Wakazi

Mwanamke waBenin.

Wataalamu wengi wanakubaliana kutambua Afrika kama asili yabinadamu wote walioko duniani.[9]

Mwaka 2010 idadi ya wakazi wa nchi zote za Afrika ilipitabilioni 1. Ni kwambaidadi yao imeongezeka sana katika miaka 40 iliyopita, ikipiku zile zaUlaya naAmerika.

Ilhali mwaka1950 walikuwepo Waafrika milioni 229 pekee, idadi iliongezeka kuwa milioni 630 mwaka1990 na milioni 1200 mnamo2014.[10][11]

Hivyoasilimia yawatoto navijana ni kubwa. Kuna nchi kadhaa ambako zaidi yanusu ya wananchi wako chini yaumri wa miaka 25.[12] Wakazi wa Afrika ni vijana kuliko wale wa mabara mengine yote;[13][14] mwaka2012 umri wa wastani ulikuwa miaka 19.7, wakati kidunia ulikuwa 30.4.[15]

Lugha

Makala kuu:Lugha za Afrika
Ramani ya lugha za Afrika:     Lugha za Kiafrika-Kiasia     Lugha za Austronesia     Lugha za Kihindi-Kiulaya     Lugha za KhoisanLugha za Kikongo-Kiniger:     Lugha za Kibantu     Lugha za Kisudani za Kati na Mashariki     Central Bantoid     Eastern Bantoid     Guinean     Lugha za Kimande     Western BantoidLugha za Kinilo-Sahara:     Kanuri     Nilotic     Lugha za Kisonghai

Zaidi yalugha elfu za Kiafrika zinazungumzwa barani leo, ingawa nyingi zinazidi kufifia.

Kusini mwa Afrika,Afrika Mashariki naya Kati watu wengi ni wasemaji walugha za Kibantu (kwa mfanoKiswahili). Asili yao ilikuwa pande za kusini zakanda ya Sahel na kutoka kule walienea katika sehemu nyingi za Afrika upande wa kusini kwa Sahara.[16]

Kuna pia vikundi vya wasemaji walugha za Kinilo-Sahara waliofika hadi Afrika ya Mashariki.

Wakazi asilia siku hizi wako wachache, wakionekana kama wasemaji walugha za Khoisan au zaWabilikimo.[17]

Watu wa Afrika Magharibi husema zaidiLugha za Kiniger-Kongo hasa zisizo za Kibantu, pamoja na wasemaji wa lugha za Kinilo-Sahara.

Watu waAfrika ya Kaskazini kiasili walikuwa hasa wa makundi matatu:

  • Waberber upande wa magharibi
  • Wamisri upande wa mashariki
  • wasemaji wa lugha za Kinilo-Sahara

Waarabu waliovamia eneo hilo lote tangukarne ya 7BK wameleta lugha yao pamoja nadini yaUislamu. Lugha yao imekuwa lugha ya watu wengi siku hizi. Wasemaji waKiberber bado wako wengi kidogoMoroko naAlgeria na wachache katika sehemu zaTunisia naLibya.[18]

Kutokana naukoloni,lugha za Kihindi-Kiulaya zinazumgumzwa pia, hasaKiingereza,Kifaransa naKireno.

Kiafrikaans ni lugha ya pekee yaAfrika Kusini yenye asili yaUlaya.

Katika kisiwa cha Madagaska kwenye Bahari ya Hindi, inatumika lugha yaKimalagasy, ambayo ni kati yalugha za Austronesia.

Dini

Ramani ya dini barani Afrika.

Waafrika wanaimani za dini nyingi tofauti, lakinitakwimu zinazotolewa hazina hakika, pia kwa sababu suala hilo ni nyeti kisiasa kwaserikali zenye mchanganyiko mkubwa wa watu, kama vileNigeria,Ethiopia naTanzania.[19][20]

Kadiri yaWorld Book Encyclopedia,Islam ndiyo inayoongoza, ikifuatwa naUkristo. Kumbe kadiri yaEncyclopedia Britannica, 45% za wakazi niWakristo, 40% niWaislamu na 10% wanafuatadini asilia za Kiafrika. Wachache tu niWahindu,Wabuddha,Wabaha'i au hawana dini yoyote.

Tazama pia

Afrika portal

Tanbihi

  1. Georges, Karl Ernst (1913–1918)."Afri". Katika Georges, Heinrich (mhr.).Ausführliches lateinisch-deutsches Handwörterbuch (kwa German) (tol. la 8th). Hannover. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2016-01-16. Iliwekwa mnamo20 Septemba 2015.{{cite encyclopedia}}:Unknown parameter|= ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: location missing publisher (link) CS1 maint: unrecognized language (link)"Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2016-01-16. Iliwekwa mnamo2016-03-01.
  2. Lewis, Charlton T.; Short, Charles (1879)."Afer".A Latin Dictionary. Oxford: Clarendon Press. Iliwekwa mnamo20 Septemba 2015.{{cite encyclopedia}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Edward Lipinski,Itineraria Phoenicia, Peeters Publishers, 2004, p. 200.ISBN 90-429-1344-4.
  4. Drysdale, Alasdair and Gerald H. Blake. (1985)The Middle East and North Africa, Oxford University Press US.ISBN 0-19-503538-0.
  5. Lewin, Evans. (1924)Africa, Clarendon press
  6. (1998)Merriam-Webster's Geographical Dictionary (Index), Merriam-Webster, pp. 10–11.ISBN 0-87779-546-0.
  7. Hoare, Ben. (2002)The Kingfisher A-Z Encyclopedia, Kingfisher Publications. p. 11.ISBN 0-7534-5569-2.
  8. "Africa: Environmental Atlas, 06/17/08."Ilihifadhiwa 5 Januari 2012 kwenyeWayback Machine.African Studies Center, University of Pennsylvania. Accessed June 2011.
  9. Homo sapiens: University of Utah News Release: Feb. 16, 2005Ilihifadhiwa 24 Oktoba 2007 kwenyeWayback Machine.
  10. "Past and future population of AfricaIlihifadhiwa 24 Septemba 2015 kwenyeWayback Machine.". Source: United Nations, Department of Economic and Social Affairs, Population Division (2013).
  11. UNICEF Report: Africa's Population Could Hit 4 Billion By 2100.National Public Radio (NPR). 13 August 2014.
  12. "Africa Population Dynamics". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2015-02-17. Iliwekwa mnamo2016-02-29.
  13. http://www.washingtonpost.com/news/wonkblog/wp/2015/08/17/5-ways-the-world-will-look-dramatically-different-in-2100/
  14. Harry, Njideka U. (11 Septemba 2013)."African Youth, Innovation and the Changing Society".Huffington Post.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. ABDOULIE JANNEH (Aprili 2012)."item,4 of the provisional agenda - General debate on national experience in population matters: adolescents and youth"(PDF).UNITED NATIONS ECONOMIC COMMISSION FOR AFRICA. Iliwekwa mnamo15 Desemba 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  16. Luc-Normand Tellier (2009). "Urban world history: an economic and geographical perspective". PUQ. p. 204.ISBN 2-7605-1588-5
  17. "Pygmies struggle to survive in war zone where abuse is routine"Ilihifadhiwa 25 Mei 2010 kwenyeWayback Machine..Times Online. December 16, 2004.
  18. "Q&A: The Berbers".BBC News. 12 Machi 2004. Iliwekwa mnamo30 Desemba 2013.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  19. "African Religion on the Internet"Ilihifadhiwa 9 Mei 2008 kwenyeWayback Machine.,Stanford University
  20. Onishi, Normitsu (Novemba 1, 2001)."Rising Muslim Power in Africa Causing Unrest in Nigeria and Elsewhere".The New York Times. Iliwekwa mnamo2009-03-01.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Marejeo

Viungo vya nje

Historia
Habari
Jiografia
Historia
Siasa
Demografia
Uchumi
Utamaduni wa Kiafrika
Michezo
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Afrika&oldid=1366124"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp