Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Mungu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mabadiliko ya uandishi waherufi nne zaKiebraniaYHWH, jina maalumu la Mungu katikaBiblia ya Kiebrania.
Jina laAllah, Mungu, kwa herufi zaKiarabu.
Alama yaWasumeri iliyomaanishadingir,mungu (mmojawapo).

Mungu nijina lenyeasili yaKibantu linalotumika kwa yeyote anayesadikiwa katikadini mbalimbali kuwa nauhai wa hali ya juu.

Kati yawafuasi wadini hizo, wengi wanaona kuwaUmungu, kwa jinsi ulivyo au unavyofirika, haukubali mgawanyiko. Hasa katikaUyahudi,Ukristo naUislamu wanasisitizaumoja wa Mungu kuwa ndiomsingi waimani yao. Kwao Mungu ni wamilele, anafahamu yote na kutaka hasa uwepo waviumbe. Tena kwahiari yake alipendakujifunua kwabinadamu; kielelezo ni Ibrahimu/Abrahamu aliyefanywarafiki yake nababa wa waamini wote.

Kunadini nyingine zinazokubali kuwepo kwamiungu mbalimbali (wawili au zaidi). Hasa dini nyingiza jadi zinaamini wingi wa miungu. Dini kubwaduniani inayosadiki miungu mingi niUhindu. Pia katika sehemu zaAfrika ya Magharibiibada za miungu mingi zinaendelea hadi leo.

Mungu na miungu katikadini asilia za Kiafrika

Jamii zaAfrika zilikuwa na dini zao ambamo tunaweza kuona imani katika nguvu za kiroho ambazo zinaitwamajina tofauti. Tunaweza kukuta imani ya Mungu Mkuu, pia yamiungu mbalimbali, pamoja na imani ya kuwepo kwa roho za wahenga, mizimu napepo mbalimbali.

Tukijiuliza juu ya uhusiano kati ya mizimu, roho, miungu mbalimbali na Mungu Mkuu, ni lazima kwanza tujue imani za jadi hutofautiana kutoka jamii moja hadi jamii nyingine.

Mara ningi imani za Kiafrika humwona Mungu Mkuu mmoja kuwa wa juu na mwenyenguvu zaidi. Yuko kabla ya kilakitu kingine naasili yake haijulikani. Hivyo nguvu hutazamwa kwangazi tofauti;Mwenyezi Mungu yuko juu, chini yake kuna roho mbalimbali au hata miungu pamoja na nguvu za asili, na mwishoni binadamu wasio na nguvu nyingi.

Wakati mwinginehadithi zauumbaji za Kiafrika zinamwonyesha Mungu akiwa au akienda mbali na watu au hawasiliani nao tena moja kwa moja. Anaacha washughulikiwe na roho au miungu midogo aliyoumba pia. Mungu wa aina hiyo anaonekana mbali sana na mambo ya binadamu; kwa sababu hiyo, mara kwa mara miungu midogo huombwa badala yake ili kupata usaidizi. Katika jamii nyingine wanaamini kwamba mizimu inaweza kuletamawasiliano baina ya Mungu na binadamu.

Vikundi vingine humwona Mungu Mkuu kuwa karibu sawa na miungu mingine, kamamwenyekiti wao au kamamfalme kati yamachifu.Wafon katikaAfrika ya Magharibi humwaza Mungu mkuu kamamapacha mawili: Mavu, nguvu ya kike, na Lisa, nguvu ya kiume. Wakitazamwa kama nguvu moja huitwa Mavu pekee. Wameumbawatoto ambao hutawala shughuli zadunia na viumbe vyake kama miungu.

Dhana za aina hiyo zimeleta majadiliano kati ya wataalamu kuhusu kuainisha dini za Kiafrika kuwa zaMungu mmoja (monotheistic) au za miungu mingi (polytheistic). Wengine huona uainishaji huo hauna maana kwa dini za Kiafrika.

MtaalamuJohn Mbiti waKenya aliona kwamba kimsingi imani katika Mungu mmoja inapatikana kwa namna moja au nyingine katika dini zote za asili. Anaeleza nguvu nyingine za kiroho kamatabia au shughuli za Mungu yeye yule zinazotazamwa pekepeke.

Mungu katika Biblia

Biblia inaanza kwa kukiri kwambaasili ya uhai wote ni Mwenyezi Mungu: “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi” (Mwa 1:1).

Mesha Stele nijiwe la zamani lililoandikwa mwaka840 KK na ni ushahidi wa kwanza kufahamika wa Mungu wa Israeli,Yahweh.

Tena, kwamba Mungu anazidi kushughulikia viumbe vyake, akividumisha na kuviongoza vyote vifikie lengo alilovipangia. “Ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda na kuwa na uhai wetu” (Mdo 17:28). Tunamtegemea pande zote: angetuacha kidogo tungetoweka mara.Yesu alipolaumiwa kwakuponyawatu siku yapumziko, alijitetea kwamba, “Baba yangu anatendakazi hata sasa, nami ninatenda kazi” (Yoh 5:17). "Yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu" (1Pet 5:7).

Kutokana naimani hiyo, tunahimizwa kujiachiliamikononi mwake kwamoyo wakitoto, tukiwajibika bila mahangaiko yanayowapata watu wasiomjua. “Waangalienindege waangani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wambinguni huwalisha hao. Ninyi je, si bora kupita hao?” (Math 6:26). “Nawe una nini usichokipokea?” (1Kor 4:7). “NimrudishieBwana nini kwa ukarimu wake wote alionitendea?” (Zab 116:12).

Tunaanza kumjua Mungu kwa kuzingatia viumbe vyake, hasadhamiri yetu. “Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake” (Rom 1:20).

Hivyo tunaweza pia kusema juu ya Mungu kuanziawema,ukweli nauzuri wa viumbe vyake na kumsifu kiasi chetu kwamba ndiye wema, ukweli na uzuri wenyewe. Lakini tukiri pia kuwa maneno yetu duni hayawezi kutosha kamwe kufafanua fumbo lake. “Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua” (Ayu 42:3). Tungemuelewa, asingekuwa Mungu.

Mwenyezi Mungu ni ukamilifu mtupu usio na mipaka kwa milele yote. “Tazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui; hesabu ya miaka yake haitafutiki” (Ayu 36:26). “Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli” (Yoh 4:24).

AkiwaRoho, viungo ambavyo pengine anapewa vinamaanisha tu sifa fulani: k.mf.machoujuzi wake, mikonouwezo wake,mabawaulinzi wake, n.k. “Roho haina mwili na mifupa” (Lk 24:39).

Hasa Mungu amejifunua kuwaupendo wenyewe. “Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli” (Kut 34:6). “Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake” (1Yoh 4:16). “Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo” (1Yoh 4:8).

Marejeo

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Mungu&oldid=1381405"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp