Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Muhamad VI

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mohammed VI (kwaKiarabu: الملك محمد السادس للمغربal-malik muhamad as-saadis lil-maghrib yaani "mfalme Muhamad wa sita kwa Moroko") nimfalme waMoroko. Anaitwa pia "Muhamad Ben Al-Hassan".

Amepokea cheo cha mfalme tarehe23 Julai1999 masaa machache baada yakifo cha baba yake, mfalmeHassan II. Yeye ni mfalme wa 18 katikafamilia yaWaalawi anayetawala nchi hii.

Utoto na masomo

[hariri |hariri chanzo]

Alizaliwa mjiniRabat tarehe21 Agosti1963 kamamtoto wa pili na mwana wa kwanza wa mfalme Hassan II namke wake wa piliLatifa Hammou. Alisomasheria kwenyechuo kikuu cha Rabat akachukuadigrii ya kwanza mwaka1985. Akaongeza masomo hukoUfaransa na kupokeashahada la daktari tarehe29 Oktoba1993 kwenye chuo kikuu chaNizza kwa utafiti kuhusu „Ushirikiano kati yaUmoja wa Ulaya nanchi za Maghreb".

Siasa mpya

[hariri |hariri chanzo]
Mohammed VI wa Moroko akikutana narais waMarekaniGeorge W. Bush hukoofisini mwake katikaNyumba Nyeupe yaWashington DC tarehe23 Aprili2002.

Mohammed VI ameanzasiasa yamageuzi. Mara baada ya kupokea cheo alihutubia wananchi akaahidi kupambana narushwa naumaskini, kujengauchumi wa kisasa na kuimarishahaki za wananchi.

Anapingwa naWaislamu wenye mwelekeo wa kidesturi hasa kwa sababu ya sheria mpya ya familia iliyopanua haki zawakinamama tangu mwaka2004.

Ndoa yake

[hariri |hariri chanzo]

Tarehe21 Machi2002alimwoamtaalamu wakompyutaSalma Bennani aliyezaa mtoto wa kwanzaMulai Hassan ambaye nimfalme mteule wa Moroko.

Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Muhamad_VI&oldid=1082462"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp