Mtolondo
Zana
Kijumla
Chapa/peleka nje
Miradi mingine
Mtolondo | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Dume laMtolondo domo-jekundu | ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 11:
|
Mitolondo aubwerenda nindege wadogo wajenasiLagonosticta katikafamiliaEstrildidae ambao wanatokeaAfrika tu. Wanafana namishigi lakini madume wana rangi za nyekundu, kahawa na kijivu, pengine pamoja na madoa meupe madogo. Majike wana rangi za kahawa na kijivu kwa kawaida lakini mara nyingi wana sehemu nyekundu pia na madoa meupe kidarini. Hulambegu hasa nawadudu pia, hususa makinda. Tago lao ni tufe lamanyasi namajani lenye mwingilio kwa kando. Jike huyatagamayai 3-6. Spishi nyingi ni wateswa wavinili ambao huyataga mayai yao katika matago ya mitolondo.