Stempu ya Kirusi mnamo mwaka 1977 inayotangaza matumizi ya misimbo ya postaSehemu za msimbo wa posta wa Kanada (herufi + tarakimu)
Msimbo wa posta (piapostikodi)[1] (ing.post code,ZIP auPIN) ni ufutanao watarakimu au herufi unaotaja eneo ambakobarua inatakiwa kufikishwa.
Siku hiziposta za nchi nyingi za dunia hutumia misimbo hii. Kusudi lake ni kurahisisha kazi ya kuchambua na kutenganisha barua zinazopokelewa kufuatana na mahali zinapotumwa. Si lazima tena mfanyakazi wa posta ajue mahali pengi inatosha kugawa barua kufuatana na misimbo iliyoandikwa kwenye bahasha. Kwa hiyo misimbo hupangwa kufuatana na utaratibu wa kugawa na kusafirisha barua.
Kwa matumizi ya teknolojia ya kisasa kuna pia mashine zinazochambua barua zikitambua namba kwenye bahasha.
Kwa mfano barua kwa mteja hukoNairobi-Westlands awe na msimbo wa posta 00800, halafu jina na namba ya sanduku la posta; kwa mteja huko Ololulunga katika Bonde la Ufa msimbo ni 20503.
Vivyo hivyo katika Tanzania barua kwendaKashaulili hukoMpanda katikaMkoa wa Katavi iwe na msimbo 50106; mfanyakazi hahitaji kukumbuka jina na kata hii inatosha akiona msimbo uananza kwa tarakimu 5 ataweka bahasha katika kikapu cha Katavi.