Msanidi programu, aumhandisi programu,msanidi kompyuta aukoda (kutokaKiingerezaprogrammer, computer programmer, software developer, software engineer aucoder) ni mtu anayeundaprogramu za kompyuta[1].
Msanidi programu huunda programu ya kompyuta kwa kutoa maelekezo (kupitialugha ya programu husika) kwakompyuta, au kwa kusanidimsimbo chanzo uliopo. Wasanidi programu wengi wana uzoefu mkubwa kwenye mahesabu na uandishi wa misimbo chanzo kwa kutumia lugha za programu mbalimbali kama vilePHP,C,C++,Python,JavaScript, auSQL.
Wasanidi programu waliojikita kuunda programu zawavuti hupenda kujiita wasanidi wavuti (kutoka kwenye kiingerezaweb developer auweb programmer).
Hakuna neno rasmi lililoteuliwa, hivyo neno "msanidi programu" na "mhandisi programu" yanaweza kuwa na majukumu sawa kwenye baadhi yamakampuni, kwa kawaida mtu mwenye jina kazi la "msanidi programu" au "msanidi" kazi yake kubwa ni kubadili maelezo ya kina ya mfumo kuwa msimbo chanzo utakaoeleweka na kuchakatwa na kompyuta, kurekebisha makosa na kuhakiki msimbo chanzo. Anaweza kuwa nastashahada yasayansi kompyuta, stashahada, aliyejifunza mwenyewe, au aliyehudhuria kambi zinazotoa masomo ya uandishi programu au mafunzo ya mtandaoni. Yule mwenye kazi jina la "mhandisi programu" anatarajiwa kuwa na uelewa mpana kuhusu sheria na kanuni zauhandisi,hisabati na njia zakisayansi.
Mchoro wa Ada Lovelace, mwanahisabati wa kiingereza anayetambulika na wengi kama msanidi programu wa kwanza.
Mwanahisabati wa kiingerezaAda Lovelace, ndiye anayetambulika na wengi kama msanidi wa kwanza wa programu kwasababu aliandikaalgoriti ya kwanza ya kukokotoanambari za Bernoulli, algoriti iliyopaswa kuchakatwa na injini ya uchanganuzi yaCharles Babbage[2] ambayo kwa wakati huo ilikua bado haijaundwa.
Wanachama wa timu ya upangaji programu (Kingereza:programming) yaENIAC ya mwaka 1945, Kay McNulty, Betty Jennings, Betty Snyder, Marlyn Wescoff, Fran Bilas na Ruth Lichterman, ndiyo wanajulikana kama wasanidi programu wa kwanza wa kulipwa.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuMsanidi programu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.