Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Moroko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Moroko
المملكة المغربية (Kiarabu)
ⵜⴰⴳⵍⴷⵉⵜ ⵏ ⵍⵎⵖⵔⵉⴱ
Kaulimbiu: ٱللَّٰه، ٱلْوَطَن، ٱلْمَلِك ("Mungu, Nchi, Mfalme")
Wimbo wa taifa: "an-Našīd al-Waṭanīy"
Eneo la Moroko katika Afrika ya Kaskazini MagharibiEneo la Moroko katika Afrika ya Kaskazini Magharibi
Mji mkuu
na mkubwa
Rabat
Lugha rasmiKiarabu,Tamazight
Dini
UraiaMmoroko
SerikaliUfalme wa kikatiba wa bunge wa umoja
  Mfalme
Mohammed VI
  Waziri Mkuu
Aziz Akhannouch
  Ufalme wa Idrisid
788
  Nasaba ya 'Alawi (nasaba ya sasa)
1631
  Ulinzi wa Ufaransa
30 Machi 1912
  Uhuru
7 Aprili 1956
Eneo
  Jumlakm2 446,550 km²(ya ya 57)
  Maji (asilimia)0.056% (250 km²)
Idadi ya watu
  Kadirio la 202437,493,183
  Msongamano79.0/km²/km2
PLT (PPP)Kadirio la 2024
  Jumla $396.685 bilioni(ya 56)
  Kwa kila mtu $10,615(ya ya 120)
PLT (Kawaida)Kadirio la 2024
  Jumla $157.087 bilioni
  Kwa kila mtu $4,203
HDI (2022)0.698
Gini (2015)40.3
SarafuDirham ya Moroko (MAD)
Majira ya saaUTC+1,UTC+0 (wakati wa Ramadhani)
Upande wa magariKulia
Msimbo wa simu+212
Jina la kikoa.ma,.المغرب
Ramani ya Moroko -mpaka wakusini haueleweki kimataifa

Moroko (piaMaroko, kwaKiarabu المغرب), rasmi kamaUfalme wa Moroko, ni nchi katikaAfrika ya Kaskazini, inayopakana naBahari ya Atlantiki naBahari ya Mediteranea kaskazini,Algeria mashariki, na Sahara Magharibi kusini. Ina idadi ya watu takriban milioni 37, ikiwa ya 40 duniani. Jiji lake kubwa zaidi niCasablanca, wakati mji mkuu niRabat. Moroko imegawanyika katika mikoa 12, inayosimamia utawala wa ndani wa nchi. Inajulikana kwa historia yake tajiri ya kifalme, miji ya kihistoria kama Fez na Marrakesh, na urithi wake wa kipekee unaochanganya tamaduni za Kiarabu, Berber, na Ulaya.

Jina

Jina la "Moroko" limetokana namji mkuu wa kaleMarakesh.

Jiografia

Pwani ya Moroko jinsi inavyoonekana kutokaHispania kupitiamlango wa bahari waGibraltar.

Eneo la Moroko nikm² 446,550. Sehemu kubwa nijangwa laSahara. Watu walio wengi huishi kwenye sehemu zarutuba karibu na pwani.

Kunamilima inayofunika maeneo makubwa. Milima yaRif inaongozana na pwani ya Mediteranea yenye mwelekeo kutoka kaskazini-magharibi kwenda kaskazini-mashariki. Milima yaAtlas iko katikati ya nchi kutoka kusini-magharibi kwenda kaskazini-mashariki.

Miji mikubwa

Mji mkuu niRabat wenye wakazi milioni 1.2.Mji mkubwa niCasablanca (kwa Kiarabu: الدار البيضاء dar al-baiDa = nyumba nyeupe). Miji yote miwili mikubwa ni miji yabandari.


Miji mitano mikubwa ni kama ifuatavyo (namba zasensa ya mwaka2004):

Historia

Makala:Historia ya Moroko

Moroko ya Kale

Habari za kimaandishi za kwanza ni kutokakarne za kwanzaKK.Wafinisia walijenga miji yao pwani lakini eneo la ndani lilibaki nchi yaWaberber walioundaufalme wa Mauretania ya Kale (usiuchanganye na nchi ya kisasaMauretania) uliounganisha sehemu kubwa ya Moroko ya kaskazini.

Wamauretania wa kale walishirikiana naDola la Roma hadi kuwa jimbo la dola hili kwa jina la "Mauretania Tingitana".

Wakati wa kudhoofika kwa Dola la Roma kuanzia mwaka400BK kukawa nauvamizi waWavandali.

Uvamizi wa Kiarabu

Karne ya 7BK ilileta uvamizi waWaarabu walioteka nchi na kusababisha polepole Waberber (waliokuwaWayahudi,Wakristo au wafuasi wadini za jadi) kuwaWaislamu.

Mwanzoni Moroko ilikuwa sehemu yamilki ya khalifa yaWaomawiyya waliotawalaDameski (Siria). Baada ya kupinduliwa kwa Waomawiyya naWaabasiya waBaghdad (Iraq) mkimbizi MwarabuIdris ibn Abdallah (788-791) alikusanya makabila ya Waberber na kuunda milki ya kujitegemea. Hii ilikuwa mwanzo wa Moroko kuwa milki ya Kiislamu inayojitawala.

Watawala wa kienyeji

Vipindi vyahistoria husebabiwa kufuatana na familia zilizofuatana za wafalme Waarabu au Waberber.

Eneo la utawala wa Wamurabitun

Moroko ilitawaliwa na familia za (miaka BK)

Murabitun na Muwahidun

Wafalme waWamurabitun (Almoravi) (1073-1147) na waWamuwahidun (Almohad) (1147-1269) walienezautawala wao hadiAfrika ya Magharibi (Mauretania,Senegal naMali ya leo) na sehemu kubwa yaAndalusia (Hispania ya Kiislamu), tena hadi mipaka yaMisri.

Wamuwahidun waliendelea kupanuka kuelekeaMisri lakini baadaye walidhoofika wakapaswa kuwaachia Wahispania Wakristo sehemu zaAndalusia.Athira ya milki ya Moroko ilipungua baadaye hadiHispania yote ikarudishwa kwa watawalaWakristo mwaka1492; pia utawala kusini kwaSahara haukuendelea.

Wareno waWahispania waliendelea kuteka miji kwenye pwani za Moroko. Utawala wa Hispania juu yaCeuta naMelilla leo ni mabaki ya nyakati zile.

Sehemu za nchi zilianza kujitawala bila kukubali tena mamlaka wa juu, kwa mfano makabila ya Waberber milimani au miji ya Rabat naSale iliyounda dola dogo laJamhuri ya Bou Regreg katikakarne ya 17 na kujishughulisha nauharamia.

Waalawi (1666 hadi leo)

Katikakarne ya 17familia ya Waalawi walishika mamlaka wakaendelea nayo hadi leo. Waliweza kutunzauhuru wa nchi hadi mwanzo wakarne ya 20. Lakini mwanzo wa karne ya 20Ufaransa naHispania walimlazimishamfalmeMulay Abdelaziz kukubalimkataba uliofanya Moroko kuwa kamakoloni chini ya nchi hizo mbili.

Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilidhoofisha Ufaransa pamoja na kuingia kwawanajeshiWaamerika naWaingereza naahadi zao za kuleta uhuru tokeo lililohamasishawazalendo wa Maroko kupigania upya uhuru wa nchi.

Baada yavita Wafaransa walijaribu kukandamiza mwendo huo wakamwondoaSultaniMohammed V nchini1953.Ghasia zikaongezeka, Sultani akarudi na nchi ikapewa uhuru mwaka1956.

Utawala wa mwanaeHassan II kuanzia mwaka1961 uliitwa "miaka ya risasi" kwa sababu mfalme alikataa kukubali utaratibu wa kidemokrasia.Chaguzi zilikuwa zauwongo,wapinzani wakatupwajela au kuuawa. Hassan II alishinda majaribio mbalimbali ya kumpindua.Siasa ya kushikamana naMarekani ilimsaidia mfalme kimataifa lakini baada ya mwisho wa "vita baridi" alilazimishwa na Wamarekani kulegeza utawala wake.

Mtoto wakeMuhamad VI akawa mfalmekijana mwaka1999 akaanza mageuzi ya kisiasa ya wazi zaidi.

Demografia

Mnamo 60 % (Januari2005) za wakazimilioni 32.7 huishi mijini.

Kiasili wakazi wengi niWaberber naWaarabu, pamoja na watu wa asili yaAndalusia (Hispania) na waAfrikakusini kwa Sahara. Waberber ndio wenyeji asilia.

Kaskazini mwa nchi ambakokitovu chake niFes kuna zaiditabia ya Kiarabu, wakatu kusini ambako kitovu chake ni Marakesh kuna tabia ya Kiberber zaidi.

Lugha

Lugha rasmi ya nchi niKiarabu naKiberberi. Waberber wengi, hasa kaskazini, wameacha lugha yao na kutumia Kiarabu lakini walileta maneno yao katikalahaja ya Kiarabu cha Kimaroko. HataKifaransa kinatumika sana.

Dini

Uislamu ndiodini rasmi na ndio unaofuatwa na wakazi wengi sana (98.9%), hasaWasunni. Wengine niWakristo (0.9%) naWayahudi (0.2%). Wakristo karibu wote ni wa asili yaUlaya. Wayahudi waliwahi kuwa wengi kidogo, lakini idadi yao imepungua katika miaka ya nyuma kutokana nauhamaji hata kama hali yao katikataifa ni nzuri kulingana na nchi nyingine za Kiarabu.

Uchumi

Nguzo za uchumi wa nchi ni kilimo na magodi ya kuchimba madini, pamoja na uvuvi na utalii.

Zaidi ya asilimia 40 za wananchi hulima. Kwa jumla asilimia 18 za eneo la Moroko zinatumiwa kwa kilimo, hasa katika magharibi na kaskazini-magharibi.

Nchi hii ina akiba kubwa ya fosfati inayochimbwa na kuuzwa nje kwa matumzi ya mbolea. Akiba ya fosfati ni kubwa duniani. Moroko ina nafasi ya tatu katika uzalishaji baada ya China na Marekani[1].

Umuhimu wautalii kwa uchumi umezidi kukua; mwaka 2018 idadi ya watalii ilifikia milioni 12.3[2]Vivutio vya kitalii ni pamoja na mahali paurithi wa dunia kama vile


Tazama pia

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Nchi zaAfrikaBara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) |Afrika Kusini |Algeria |Angola |Benin |Botswana |Burkina Faso |Burundi |Cabo Verde |Chad |Cote d'Ivoire |Eritrea |Eswatini |Ethiopia |Gabon |Gambia |Ghana |Guinea |Guinea Bisau |Guinea ya Ikweta |Jibuti |Kamerun |Kenya |Komori |Kongo (Jamhuri ya) |Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) |Lesotho |Liberia |Libya |Madagaska |Malawi |Mali |Misri |Morisi (Visiwa vya) |Mauritania |Moroko |Msumbiji |Namibia |Niger |Nigeria |Rwanda |Sahara ya Magharibi |Sao Tome na Principe |Senegal |Shelisheli |Sierra Leone |Somalia |Sudan |Sudan Kusini |Tanzania |Togo |Tunisia |Uganda |Zambia |Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje yaAfrika
Hispania:Kanari·Ceuta·Melilla |Italia:Pantelleria·Pelagie |Ufaransa:Mayotte·Réunion |Uingereza:·St. Helena·Diego Garcia |Ureno:Madeira
Nchi wanachama waUmoja wa Afrika (AU)
Makala hii kuhusu maeneo yaAfrika bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuMoroko kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
  1. Phosphorus A Looming Crisis, Vaccari, David A. (2009). "Phosphorus: A Looming Crisis" (PDF). Scientific American. 300 (6): 54–9.
  2. Over 12 Million Tourists Visited Morocco in 2018 Bazza, Tarek (2019). "Over 12 Million Tourists Visited Morocco in 2018, Up 8% from 2017". Morocco World News. Retrieved 2019-03-21.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Moroko&oldid=1444770"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp