Monsuni hufuata mfumo wa msingi wafizikia: nchi kavu hushikajoto kutoka kwajua haraka zaidi kulikomaji. Tofauti yahalijoto kati ya nchi kavu na bahari kwenyepwani unaweza kufikia kiwango chasentigredi 20°C. Kwa mfano halijoto kwenye nchi kavu hukoUhindi inaweza kufikia mnamo 45°C ilhali maji ya karibu katikaGhuba ya Bengali naBahari Arabu ina halijoto ya sentigredi 23-25 pekee.Joto la nchi kavu linapashiamotohewa juu yake na hewa joto inapanda juu. Nafasi ya hewa inayopanda juu inachukuliwa na hewa baridi zaidi kutoka juu ya uso wa bahari. Hewa hii inabeba unyevu ndani yake inayoanza kutonesha kama mvua unaojulikana kama monsuni.
Hewa joto juu ya nchi kavu inaendelea kupanda juu na kusababisha eneo la kanieneo ya hewa duni na hii inasababisha upepo wa kuendelea kutoka baharini kuelekeabara.[3]
Usimbishaji unaimarishwa namilima inayolazimisha hewa yenye unyevu kutoka uso wa bahari kupanda juu.[4]
Milima ya Ghat kwenye pwani ya magharibi ya Uhindi wakati wa Mei 2010 (majira ya monsuni ya kaskazini).Milima ya Ghat kwenye pwani ya magharibi ya Uhindi wakati wa Agosti 2010 (majira ya monsuni ya kusini).
Wakati wabaridi nchi kavu hupoa haraka kuliko bahari inayoweza kutunza joto vizuri zaidi kwa muda mrefu. Hivyo eneo la kanieneo la hewa juu linatokea barani Uhindi wakati wa baridi na sasa upepo unageuka kupuliza kutoka bara Hindi kwenda baharini na upepo huu ni kavu.
Upepo wa monsuni unajengatabianchi ya maeneo yanayoathiriwa nao inayoitwa pia "tabianchi ya monsuni".
Monsuni inaleta mvua nyingi ambayo mahali pengi ni msingi wamisitu. Mabadiliko ya monsuni yanaweza kuleta amaukame mbaya au mvua kali zinazosababisha matatizo katikajamii.
Kwa hiyo monsuni ni muhimu kwakilimo namaisha ya watu katika maeneo yanayoathiriwa nayo. Hasa katika nchi zinazozungukaBahari Hindi majira ya monsuni yalikuwa msingi wabiashara kwa njia za bahari na kubadilishana kwa tamaduni kati ya nchi mbalimbali.
Tangumilenia watu walioishi kando ya Bahari Hindi walitumia upepo wa monsuni kwasafari zao. Monsuni ya kusini -iliyoitwa "kusi" au "upepo wa kusi" naWaswahili- iliwawezesha watu wa pwani kufanya safari ndefu sana za kuvuka bahari kati ya Uhindi, Bara Arabu naAfrika ya Mashariki kwenda upande mmoja hata kwajahazi nyepesi sana, na badiliko la mwendo wa monsuni liliwawezesha kurudi tena majira yaliyofuata.
↑Neno laKiingerezamonsoon linatokana na lile laKirenomonção, lilitokana naKiarabumawsim (موسم "majira") na/auKihindi "mausam", "labda kwa kupitia piaKiholanzi cha awalimonsun".OED online
↑LinganishaA.C. Madan, Eenglish-Swahili Dictionary, London 1902;TUKI-ESD imepokea "monsuni"