Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Monrovia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Monrovia
Mji mkuu wa Liberia Monrovia


Monrovia nimji mkuu waLiberia. Eneo uliko mji huu mwanzoni liliitwa Cape Mesurado naWareno katika miaka ya 1560. Eneo hili lilianzwa kujenga mji mwaka 1822 na chama chaAmerican Colonization Society ikiwa ni makazi ya watu waliokombolewa toka utumwani nchiniMarekani.[1] Jina Monrovia lilitokana na jina la Rais wa MarekaniJames Monroe. Kwa mujibu wasensa ya mwaka 2003, Mji huu una wakazi wapatao 572,000.

Uchumi wa Monrovia unategemea zaidi bandari yake na madini ya chuma. Bidhaa kama vilesaruji,mafuta,matofali,vigae,samani, nakemikali zinatengenezwa Monrovia.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Wakati mabaharia Wareno walipowasilia Monrovia na kuuita mji huu "Cape Mesurado" tayari kulikuwa na wakazi wakiishi hapo. Watu wa kwanza kuhamia Monrovia toka nchini Marekani waliwasili mwaka 1822 katikaKisiwa cha Sherboro nchiniSierra Leone. Wahamiaji wengi walifariki baada ya kuwasili Monrovia.

Mkutano wa kutungakatiba ya Liberia wa American Colonization Society ulifanyikia Monrovia mwaka 1845.

  1. http://www.wdl.org/en/item/446/
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Monrovia&oldid=1177049"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp