Molekuli ni maungano ya kudumu ya angalauatomi mbili au zaidi. Ni pia kitengo kidogo cha kiladutu. Kama molekuli inapasuliwa ni dutu tofauti zinazojitokeza.
Atomi ndani ya molekuli hushikwa kwa nguvu yaelektroni aumuungo atomia. Maungano ya atomi katika molekuli hufuata maumbile ya atomi.Maumbile haya Kwa mfano atomi zahidrojeni huwa na nafasi moja ya kushikana na atomi nyingine,oksijeni huwa na nafasi mbili ya kushikana na atomi nyingine.Kaboni ina nafasi nne nanaitrojeni ina nafasi tatu. Hapo ni sababu ya kwambamaji ni molekuli ya H2O yaani hidrojeni ina mkono mmoja na oksijeni ina mikono miwili hivyo atomi moja ya oksijeni ikishika atomi za hidrojeni (yenye mkono moja) mbili ni molekuli thabiti na imara hakunamkono unaobaki.
Fomula ya molekuli inaeleza idadi na aina ya atomi ndani ya molekuli. Kwa mfanosukari ina formula ya C6H12O6. Maana yake ni kwamba molekuli moja ya sukari huwa na atomi 6 za kaboni, 12 za hidrojeni na 6 za oksijeni.
Makala hii kuhusu mambo yakemia bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuMolekuli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.