Kwa hiyo mimea huwa na utando wa seli wenyeselulosi. Mmea unapata sehemu kubwa yanishati kutokanuru yajua kwa njia yausanisinuru, yaani hujilisha kwa msaada wa nuru. Ndani yamajani ya mimea kunaklorofili,dutu yarangi yakijani, inayofanyakazi ya kupokea nuru na kupitisha nishati yake kwa sehemu nyingine ya mmea ambamo inatumiwa kujengamolekuli zinazotunza nishati kwa njia yakikemia na kutumiwa katikametaboli yamwili.
Mimea kadhaa imepoteza uwezo wa kutengeneza klorofili ya kutosha, hivyo inajipatia nishati kamavimelea kutoka kwa mimea au viumbehai wengine.
Mimea mingi inazaa kwa njia yajinsia, yaani kwa kuunganishaseli za kiume na kike; mara nyingi viungo vya kiume na vya kike vinapatikana ndani ya mmea mmoja. Kuna pia mimea inayozaa kwa njia isiyo ya kijinsia, kwa mfano kwa kuoteshamzizi wahewani ambao unaingia ardhini na kuendelea kama mmea wa pekee.
Mimea ni msingi muhimu kwa viumbehai wengine duniani kwa sababu sehemu kubwa yaoksijeni katikaangahewa ya dunia inatengenezwa na mimea.[1].
Makala hii kuhusu mambo yabiolojia bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuMmea kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.