Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Mizimu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mizimu inamaanisha hasaroho zilizoishi katikamwili kabla ya kuiagadunia.

Katika baadhi yadini namila inaaminika kuwa mizimu inaweza kuwa nafaida kwa watu walio hai duniani na ina uwezo wa kuwasiliana nao kwa kutumia njia mbalimbali kufuatana namazingira auutamaduni.

Kuna tofauti kati ya mizimu; pengine ni roho zabinadamu ambao hawakutimizamajukumu yao au walifanya kinyume wakati wapo duniani; pengine ni roho za watu walioshi kwauadilifu.

KatikaKanisa Katoliki na baadhi yamadhehebu mengine, mizimu inaweza kuwa yawatakatifu.

Mizimu katika jadi za Afrika

[hariri |hariri chanzo]

Watafiti mbalimbali walioangalia jamii za jadi katikaAfrika walikutaimani katika mizimu. Imani hizo hazitokei Afrika tu, maana imani za kufanana zilitambuliwa pia katikadini za jadi katikamabara mengine kama vileAsia naUlaya. Lakini kilajamii ina namna yake ya pekee ya kuwaza na kushughulikia imani hizo.

Kwalugha yaKiswahili, "mzimu" nineno linalotaja pia mahali ambapo watu huwasiliana na roho za watu waliofariki dunia zamani.

Tena baadhi ya jamii za Kiafrika huamini kuna mizimu iliyoumbwa katika hali hiyo, yaani haikuwahi kuwa binadamu hapo kwanza.

Kwa hiyo, kuna imani ya mizimu ya aina mbalimbali: mizimu ambayo ni roho za watu waliokufa na mizimu ambayo haijawahi kuwa binadamu. Kwa kuwa mizimu ni roho, hainaumbo maalumu, lakini ina uwezo wa kutokea katikamaumbile tofautitofauti kama vile mtu,mnyama,mdudu,mimea, au vitu visivyo nauhai.

Kwautamaduniwa Kiafrika, mizimu mizuri ni wahenga, yaani roho za watu ambao walipokuwa katika hali ya ubinadamu waliishi vizuri kulingana na tamaduni na matakwa ya jamii, walikuwa na sifa nzuri. Sasa ni mizimu mizuri ambayo hulenga kuilinda jamii au mtu mmojammoja dhidi ya matatizo. Hivyo, pale mtu anapokumbwa na matatizo wahenga humsaidia. Aidha, kufanikiwa au kutokufanikiwa kwa jamii katika masuala mbalimbali kunatokana na uhusiano wao na wahenga. Jamii inapaswa kufuata mila nadesturi zake na kuepuka, kadiri iwezekanavyo, kuvunjamiiko ya jamii kwa sababu kufanya hivyo kunawaudhi wahenga. Mtu anayefuata kanuni zote hulindwa, hupata mafanikio na kuishi kwaamani ilhali yule anayekiuka mila na desturi hupatwa na majanga makubwa au anaweza kuiingiza jamii nzima katika matatizo kwa sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wahenga kujitoa katikaulinzi na hivyo kuyaachia mizimu mibaya nafasi ya kufanya mambo mabaya, au wahenga wenyewe kutoaadhabu kwa jamii au kwa mtu mmojammoja.

Aidha, inasadikiwa kuna mizimu mibaya, ambayo malengo yao ni kuidhuru jamii na wakati mwingine hujitokeza kama pepo ambao huwaingia na kuwadhuru watu; hao huitwa kwamajina tofautitofauti kama vile misoha, irumenang, na’ndenga na war’umu kwaWabena,Wamasai,Wamakonde naWachaga. Baada yaUislamu naUkristo kuenea barani Afrikakusini kwa Sahara yanatumika pia majina yanatokana na lugha yaKiarabu kamamashetani aumajini ambayo kwaasili yana maana tofauti. Hao mizimu mibaya huwa na kinyume cha sifa hizo hapo juu, yaani walipokuwa binadamu waliishi katika hali isiyotakiwa katika jamii au inayochukuliwa kuwa ni ya kutiaaibu, halafu kufa katika hali inayochukuliwa kuwa ni yalaana, kama vile kujinyonga au kuzikwa bila kufuata mila na desturi za jamii. Kwa mfano,Wanyore waKenya huamini kuwamwanamume aumwanamke anayefariki dunia kabla hajaoa au kuolewa atataka kuzuia wengine kuoa au kuolewa na kuzaa. Kwa hiyo, kabla ya miili ya wanaume na wanawake hao kuzikwa, inafanyiwa miviga ili kuzuia tatizo hilo lisienee kwa wengine. Aidha, inasadikiwa kuwa baadhi ya mizimu mibaya hutokana nawatoto ambao walikufa kabla ya kuzaliwa: hao huidhuru jamii kwa sababu huwa nahasira na hutaka kulipakisasi.

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Mizimu&oldid=1252923"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp