Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Milki ya Maurya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Milki ya Wamaurya mnamo 250 KK

Milki ya Wamaurya (kwaKiing. Maurya Empire) ilikuwamilki kubwa ya kwanza katikahistoria ya Uhindi. Mlki hiyo ilianzishwa mnamo322 KK naChandragupta Maurya.

Utawala wa Chandragupta Maurya

[hariri |hariri chanzo]

Chandragupta Maurya alianzisha milki ya Maurya kwa kupinduanasaba ya Nanda na kupanuaufalme huo kwa msaada waChanakya. Kufikia316 KK, himaya ya Maurya ilitawala kabisa sehemu zaKaskazini-Magharibi zaUhindi, ikiwashinda na kuteka maeneo yaliyokuwa chini yamagavana walioachwa naAleksander Mkuu. Chandragupta Maurya alimshindaSeleukus I Nikator akapata maeneo upande wa magharibi waMto Indus.[1]

Baada ya Chandragupta Maurya, mwanaweBindusara alianza kutawala kutoka298 KK. Aliitwa "Amitraghata",neno la Kisanskrit linalomaanisha kwamba Bindusara ndiye "muuaji wa maadui". Alishinda sehemu zakusini mwa Uhindi. Baada yakifo chake, ni Kalinga tu (Orissa wa kisasa) na sehemu zaTamil Nadu zilizobaki nje ya himaya yake.

Sarafu ya alama ya fedha ya ufalme wa Maurya, na alama za gurudumu na tembo. Karne ya 3 KK.

Kipindi cha dhahabu cha milki

[hariri |hariri chanzo]

Mfalme Ashoka, mwana wa Bindusara, alikuwa mtawala wa Milki ya Maurya mnamo268 KK. Anahesabiwa kati ya watawala mashuhuri zaidi waBara Hindi. Ashoka alishinda Kalinga katikavita kali inayojulikana kamaVita ya Kalinga. Hii ndiyo vita pekee iliyopigwa na Mfalme Ashoka. Waliokufa ni zaidi ya watu 200,000. Mkoa wa Kalinga uliharibiwa na ulionekana umwagajidamu. Hii ilibadilisha mawazo ya Ashoka. Alijitoleamaisha yake yote kwa "ahinsa" na "dharma-vijaya". AkawaMbudha baada ya vita hivi.Amri zake zimehifadhiwa kamamwandishi uliochongwa katikamiamba kwenye milki yake.

Nembo ya kisasa ya Uhindi ilinakiliwa kutoka kwa moja yanguzo zake za mwamba. Kwa kawaida aliitwa Ashoka Mkuu.

Kushuka

[hariri |hariri chanzo]

Baada ya kifo cha Ashoka mnamo232 KK, milki yake ilianza kupungua. Dola hilo lilidumu miaka hamsini tu baada ya kifo chake.Brihadratha Maurya, mfalme wa mwisho wa Wamaurya aliuawa najenerali wakePushyamitra Sunga, ambaye alianzishaMilki ya Sunga mnamo185 KK.[2]

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. http://www.metmuseum.org/toah/hd/maur/hd_maur.htm
  2. "KING ASHOKA: His Edicts and His Times".www.cs.colostate.edu.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Milki_ya_Maurya&oldid=1305394"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp