Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Milki ya Britania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"Dola la Uingereza" inaelekezwa hapa. Kwa matumizi mengine, tazamaDola la Uingereza (maana).
Ramani ya nchi ambazo zilikuwa sehemu ya Milki ya Uingereza mnamo mwaka1921.

Milki ya Britania (pia:Milki ya Uingereza, ing.British Empire) ilikuwamilki kubwa ambayo ilijumlisha maeneo yaliyomilikiwa naUfalme wa Muungano. Milki hii ilikuwa himaya kubwa ya kisiasa katikahistoria nzima, na iliweza kumiliki wakati wa kilele chakerobo ya uso wadunia.

Zaidi ya watumilioni 458 walikuwa chini ya udhibiti wa seikali ya London. Leo hii, maeneo yake mengi yamekuwa nchi huru zilizo wanachama waJumuiya ya Madola.

Kiini cha milki hii kilikuwautawala waUingereza juu yaUhindi uliotajirisha nchi tawala. Mwanzoni ilikuwa kampuni ya binafsi iliyofanyabiashara huko, baadaye kutwaa maeneo hadi Uhindi yote kuwa mchanganyiko wamakoloni na "maeneo lindwa" zilizosimamiwa na washauri Waingereza kando ya watawala wenyeji.

Katika maeneo mengine Uingereza haukutafuta utawala wa moja kwa moja lakini ilitandaza nyavu za vituo vya kijeshi na kibiashara juu ya sehemu zote za dunia. Pale ambako wafanyabiashara wa Uingereza walikuwa na maslahijeshi liliingia kati kuhakikisha ya kwamba wapate faida jinsi ilivyokuwa katikaChina ambayo haikufanywa kuwa koloni lakini ililazimishwa kuruhusu biashara yamadawa ya kulevya kwa njia yavita mbili.

Katikakarne ya 19 Uingereza ilichukua pia utawala juu ya sehemu kubwa yaAfrika; ingawaserikali yaLondon ilisita mara nyingi kuchukua maeneo mapya, maslahi ya wafanyabiashara nawalowezi yalisababisha uenezaji wa himaya yake.

Katika robo ya mwisho wa karne ya 19 mashindano kati ya mataifa ya Ulaya yalisababisha kutwaliwa kwa maeneo mengine hasa kwa shabaha ya kwamba nchi nyingine isienee; kwa njia hiiKenya ikawa koloni la Uingereza.

Mwisho wa karne ya 19 Uingereza ilianza kuyapa makoloni kadhaa viwango tofauti vya kujitawala kama "dominion" kama idadi ya wakazi Waingereza ilikuwa kubwa; kwa njia hii nchi kamaKanada,Australia,New Zealand na Maungano yaAfrika Kusini zilipata serikali nakatiba zao na kiwango cha kujitawala kiliongezeka polepole hadimfalme aumalkia wa Uingereza alikuwa mkuu wa dola wa heshima bila athira juu ya siasa tena.

Baada yaVita Kuu ya Pili ya Dunia Uingereza ilikosa nguvu ya kuendelea na utawala juu ya maeneo haya makubwa. Ilipaswa kuyapa uhuru, kuanzia Uhindi na Pakistan mwaka1947 hadi nchi za Afrika tangu mwaka1960.

Makoloni kadhaa, hasa nchi zavisiwa vidogo, yaliamua kutotafuta uhuru yakaendelea kamaMaeneo ya ng'ambo ya Uingereza hadi leo. Koloni la mwisho lililorudishwa kwa nchi mama ilikuwaHongkong mwaka1997.

Visiwa vya Falkland vilisababisha vita kati ya Uingereza naArgentina mwaka1982 kwa sababu Argentina inadai visiwa kamamali yake ikapeleka wanajeshi visiwani, lakini Uingereza ulidai wakazi wa Falkland wanataka kuendelea kamaraia wa Uingereza, wakaondoa Waargentina kwa nguvu ya kijeshi.

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Madola ya Kale
Karne za Kati
Madola ya karne 5 za mwisho
Madola ya kikoloni
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuMilki ya Britania kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Milki_ya_Britania&oldid=1412146"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp