Mikosi | ||
---|---|---|
![]() | ||
Studio album yaG.W.M | ||
Imetolewa | 2000 | |
Aina | Hip hop | |
Lebo | GMC | |
Mtayarishaji | Rajabu Marijani Bonny Luv |
Mikosi, nijina laalbamu ya kwanza kutoka kwa kundi zima lamuziki wa hip hop laTemekeDar es Salaam,Tanzania maarufu kamaG.W.M. Albamu imetoka mwaka wa2000 - ukiwa mwaka wa matoleo mengi ya albamu zahip hop ya Tanzania kutoka. Hamasa ya kutoa albamu na kufanya uzinduzi zama hizi ndiyo hasa zilitamba. G.W.M ni moja kati ya makundi yanayoheshimika katika miaka ya1990.
Walikuwa kufahamika haraka nchini Tanzania kwa ujuvi wao wa utunzi wa mashairi ulioendana na wakati ule. Walianza kutamba mwaka 1995 baada ya kutoa wimbo wa "Cheza mbali na kasheshe". Albamu hii ilitakiwa itoke tangu miaka ya 1990, lakini mipango ya kusaini mkataba wake ilienda kombo na kuja kutoka mwaka wa 2000, mbele kidogo baada ya kuvuma kwa sana. KR baaaye akajiunga na kundi la muda mfupi laWachuja Nafaka. Nyimbo za katika albamu zilitayarishwa naBonny Luv naRajabu Marijani.
Hii ni orodha ya nyimbo zinazopatika katika albamu hii na maelezo yake ya msingi.
Upande | Jina la wimbo | Maelezo |
---|---|---|
A1 | Yamenikuta | Wakiwa naII Proud |
A2 | Bwana Kidevu | Wakiwa naG. Solo naMc Steav |
A3 | Mguu Nje | Wakiwa naDolla Soul |
A4 | Kipe Kitu | Ilivuta hisia kwa watu wengi wakati ule |
A5 | Mguu Nje Instru. | Midundo mitupu |
B1 | Mikosi | Wakiwa na Dre'z |
B2 | Mwenye Nyumba | Wakiwa na Dre'z |
B3 | Machizi Wangu | Wakiwa naSloughter |
B4 | Autro | |
B5 | Machizi Wangu Instru. | Midundo mitupu |