Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Microsoft

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Windows
Microsoft
IlipoanzishwaAlbuquerque,New Mexico (Aprili 4, 1975 (1975-04-04))[1]
Makao MakuuRedmond, Washington,Marekani
Mapato kabla ya riba na kodidecreaseUS$ 20.363 billion(2009)
Net incomedecreaseUS$ 14.569 billion(2009)
Total equityUS$ 39.558 billion(2009)
Tovutidjt5www.microsoft.com
Mti unaotunzwa na Microsoft karibu na ofisi ya Dell, Bangalore, India.

Microsoft Corporation nikampuni ya kimataifa yateknolojia yakompyuta.[2] NenoMicrosoft ni neno unganifu lilitokana namaneno yaKiingereza "microcomputer" na "software".

Kampuni ilianzishwa naWilliam Henry Gates III (anayefahamika zaidi kamaBill Gates) naPaul Allen 04 Aprili1977, ili kuendeleza na kuuza mifumo-ongozo rahisi kwa ajili ya kompyuta ndogo zaAltair 8800. Kampuni hili liliinuka na kutawala soko la utengenezaji wa mifumo-ongozo ya kompyuta binafsi kupitia mfumo wake unaojulikana kamaMS-DOS (Microsoft - Disk Operating System) katikati yamiaka ya 1980, ikifuatiwa na programu yaMicrosoft Windows[3].

Makao makuu yakoRedmond, Washington,Marekani.

Kampuni hii inaendeleza, kutengeneza, kutoa leseni, kusaidia na kuuzaprogramu za kompyuta, vifaa vya umeme, kompyuta binafsi pamoja na huduma zihusianazo na hizo. Programu yake ya kompyuta ijulikanayo sana ni mfumo ongozo wa kompyuta waMicrosoft Windows, na programu nyingine kama vile,Microsoft Office, naInternet Explorer pamoja naEdge Web. Vifaa vyake maarufu ni vifaa michezo vya Xbox pamoja na mfumo wakioomguso uitwaoMicrosoft Surface lineup kwa ajili ya kompyuta binafsi.

Kwa mwaka wa 2016, ndiyo kampuni kubwa duniani yenye kutengeneza programu za kompyuta kwa makusanyo ya jumla, na ni moja kati ya kampuni zenye thamani kubwa zaidi duniani. Microsoft ni kampuni iliyoko nafasi ya 31 katika orodha ya mwaka 2018 ya Fortune 500 ya mashirika makuu makubwa ya Marekani na mapato ya jumla.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Microsoft ni kampuni kubwa yateknolojia yahabari iliyoanzishwa mnamo tarehe4 Aprili mwaka1975, naBill Gates na Paul Allen huko Albuquerque,New Mexico,Marekani. Kampuni hii ilianza kama kampuni ya kuuza lugha yaprogramu ya msimbo kwakompyuta, lakini haraka ikawa mmoja wa watengenezaji wakubwa wa programu za kompyuta ulimwenguni.

Historia ya Microsoft imejaa mafanikio na uvumbuzi wateknolojia. Mwaka1985, kampuni hiyo ilizindua Windows 1.0, mfumo wa uendeshaji wa kompyuta uliofanikiwa kwa soko kwa kutumia mwonekano wa picha. Tangu wakati huo, Microsoft imekuwa ikitoa matoleo mengi ya Windows pamoja na bidhaa nyingine kama vile Microsoft Office Suite, Internet Explorer, na Xbox.

Katika miaka ya1990 na2000, Microsoft ilikuwa kiongozi katika soko laprogramu yakompyuta na inasemekana kuwa mojawapo ya kampuni zateknolojia tajiri zaidi ulimwenguni. Walakini, kampuni hiyo imekabiliwa na changamoto kadhaa za kisheria na ushindani wa soko katika miaka ya hivi karibuni.

Leo, Microsoft bado ni mojawapo ya makampuni yateknolojia yenye ushawishi mkubwa ulimwenguni, ikitoa suluhisho zaprogramu na vifaa vyakompyuta kwa watumiaji binafsi na wafanyabiashara.

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. "Bill Gates: A timeline".news.bbc.co.uk.BBC News. 2006-06-15. Iliwekwa mnamo2008-08-18.
  2. "Microsoft Corporation Annual Report 2005"(doc). Microsoft. Iliwekwa mnamo2005-10-01.
  3. "Information for Students: Key Events In Microsoft History"(doc). Microsoft Visitor Center Student Information. Iliwekwa mnamo1 Oktoba 2005.

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo yauchumi bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuMicrosoft kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Microsoft&oldid=1475208"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp