Mfumo wa homoni (kwaKiingerezaendocrine system) ni jumla yatezi zamwili zinazomwagahomoni kwenyemzunguko wa damu pamoja naogani zilizo tayari kupokea homoni hizo. Mfumo kwa jumla unaendesha kazi ya ogani za mwili.
Homoni nikemikali yaanimolekuli za pekee zinazowasilishaujumbe kwa ogani za mwili na kushawishi utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika mwili wa binadamu.
Mfumo kwa jumla unafanywa hasa na tezi za kumwaga homoni katika mzunguko wa damu lakini pia naseli kadhaa za pekee zinazotoa homoni kupitiakuta za seli kwa ogani husika moja kwa moja, kwa mfano kwamoyo,ini,utumbo na nyingine.
Mfumo wa homoni kwa lugha ya kitaalamu unaitwa "endokrini", yaani "mfumo unaomwaga ndani" kwa maana ya ndani ya mzunguko wa damu. Hii ni tofauti na tezi "exokrini" ("kumwaga nje") zinazotoa homoni aukiowevu cha pekee nje yake kupitiakichirizi hadi pale kinapotakiwa, kwa mfano tezi zajasho (kwendangozi ya nje).
Utaalamu wa mfumo wa homoni huitwa "endocrinology" ambayo nitawi laelimu ya tiba ya ndani. Mfumo wote husimamiwa na kuongozwa na sehemu yaubongo inayoitwa hypothalamus.
Makala hii kuhusu mambo yabiolojia bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuMfumo wa homoni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.