Jiji la Mexico(kwaKihispania: Ciudad de México) nimji mkuu piamji mkubwa wa nchi yaMexico. Jiji lina wilaya 16, ambazo kila moja zimegawanywa katika vitongoji aucolonias.
Mji wa Mexico ni piamkoa wa kujitegemea, huitwa mara nyingi na Wamexiko wenyewe "Mexico DF" au kwa kifupi "DF" (DF = Distrito Federal, Mkoa wa Shirikisho), lakini tangu mwaka2016 unaelekea kujitegemea zaidi kiutawala.
Idadi ya wakazi nimilioni 9, lakini pamoja na mitaa ya karibu idadi inafikia karibu milioni 20.4. Ni kati ya miji mikubwa kabisaduniani.
Kunahadithi ya kale juu ya kuundwa kwa Tenochtitlan ambao ni mji wa Kiazteki uliotangulia Mexiko City.
Zamani ile Waazteki waliishi maisha ya kuhamahama na kutafuta mahali pa kujenga mji wa kudumu.Mungu wao Huitzilopochtli aliwaambia wamtafute anayekalia mpungate (kakati) na kushikanyoka. Mpungate utapatikana kwenyemwamba katika kisiwa ziwani. Hadithi yaendelea kusema ya kwamba baada ya matembezi ya miaka 200 walikuta ziwa la Texcoco penye mwamba na mpungate. Walipokaribiatai aliyeshika nyoka akaketi kenye mpungate huu.
Baada ya kupokeaishara hiyo waliunda mji wao wa Tenochtitlan uliokuwa baadaye mji mkuu waDola la Azteki. Ulikuwa na wakazi 300,000 wakati wa kufika kwaWahispania mwaka1519.
Wenyeji wa mji waliwashambulia na kuua Wahispania wengi. Cortes aliweza kukimbia akarudi na jeshi jipya akaweza kuteka mji tarehe13 Agosti1521 na kuuharibu kabisa.
Makala hii kuhusu maeneo yaMexiko bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusuMexico (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.