Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Mercurius

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Mecurius kutoka Pompei (karne ya kwanza BK) inayomwonyesha kuwa na bawa miguuni

Mercurius alikuwa mungu wadini ya Roma ya Kale. Jina lake latokana na neno la Kilatinimerx inayomaanisha "bidhaa".

Uhusiano na mitholojia ya Kigiriki

[hariri |hariri chanzo]

Alitazamiwa na Waroma sawa na munguHermes katikamitholojia ya Kigiriki hivyo aliabudiwa kama mtume aliyebeba ujumbe kutoka mungu mmoja kwa wengine, pia kama mungu wa biashara, uchumi, mawasiliano na wezi.

Tabia zake

[hariri |hariri chanzo]

Katika mitholojia alikuwa mwana wa mungu mkuu Jupiter na mungu wa kike Maia. Tabia yake kuu ilikuwa uwezo wa kuhama haraka hivyo sanamu zake mara nyingi zilionyesha viatu na kofia yenye bawa. Mwendo wake wa haraka ilisababisha pia kumwunganisha na sayari ya kwanzaUtaridi iliyo na mwendo wa haraka kwa sababu obiti yake ni fupi kuliko sayari nyingine.

Matumizi ya jina lake katika lugha za Ulaya

[hariri |hariri chanzo]

Kwa Kilatini na lugha za Ulaya sayari hii iliitwa pia Mercurius, kwa Kiingereza "Mercury". Mercury imekuwa pia jina lametali ya zebaki kwa Kiingereza kutokana na mwendo wake wakati inamwagika.

Alitazamiwa pia kama mungu mlinzi wa siku ya "Mercurii dies" yaaniJumatano inayoitwa kwa jina lake katikalugha za Kirumi hadi leo, kwa mfano kwaKiitaliaMercoledì, kwaKifaransaMercredi, kwaKihispaniaMiércoles na kwaKiromaniaMiercuri.

Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Mercurius&oldid=1150929"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp