Meksiko, rasmiMuungano wa Madola ya Meksiko' (kwaKihispania:Los Estados Unidos Mexicanos), ninchi katikaAmerika ya Kaskazini. Inapakana naMarekani upande wa kaskazini,Guatemala naBelize upande wa kusini,Bahari ya Karibi upande wa mashariki, naBahari ya Pasifiki upande wa magharibi. Meksiko ina eneo la takriban kilomita za mraba 1,964,375, na ni miongoni mwa nchi kubwa zaididuniani. Ina mandhari mbalimbali kuanzia jangwa la Chihuahua hadi misitu ya mvua ya Yucatán, na historia tajiri inayojumuishaustaarabu wa kale kamaWamaya naWaazteki.
Ina idadi ya watu inayokadiriwa kuwa zaidi ya milioni 126 (2024), na hivyo kuwa nchi ya 10 kwa idadi ya watu duniani. Mji mkuu na mji mkubwa zaidi wamji wa Meksiko ni Mexico City, ambao pia ni kitovu chasiasa,uchumi, nautamaduni wataifa hilo. Licha ya changamoto kama ukosefu wa usawa wakijamii na usalama, Meksiko ni moja ya nchi zenyeuchumi mkubwa baraniAmerika, na ni mwanachama wa mashirika muhimu kamaUmoja wa Mataifa,G20, na Jumuiya ya Nchi za Amerika (OAS).
Watu wa kwanza waliofika huko kutoka kaskazini walikuwaWaindio, wajukuu wa wahamiaji walioingiaAmerika kutokaAsia ya Kaskazini. Hakuna uhakika kufika huko kulitokea lini: labda miaka 10,000 iliyopita[1].
Ustaarabu wa kwanza unaojulikana ulikuwa waWaolmeki baina ya 1500 KK na400 KK. Habari zao zinajulikana kutokana naakiolojia na mabaki ya miji nasanaa yao. Waolmeki walijenga miji wakaacha mifano ya sanaa yenye kiwango cha juu.
Hekalu - piramidi ya KimayaUkurasa kutoka kitabu cha Kimaya - maandishi ya hiroglifi
Sanamu nyingine inayorudirudi ni mtu-jagwaa inayounganisha sehemu yamaumbile yabinadamu najagwa. Takriban mwaka 400–300 KK miji yao iliachwa na wakazi; hakuna uhakika ni nini iliyosababisha mwisho wa ustaarabu huu.
Upande wamashariki wa Waolmeki ustaarabu waWamaya ulianza tangu takriban mwaka2000 KK. Wamaya walikaliarasi yaYucatan pamoja na Guatemala na Belize ya leo. Waliishi katika vijiji na miji iliyojitegemea na kugombana kati yao mara kwa mara.
Jamii ya Wamaya ilifikia kiwango cha juu kuanzia mwaka500 KK wakati miji mikubwa ya kwanza ilipotokea. Mnamo mwaka800BK jamii za Wamaya katika Yucatan ziliporomoka;wataalamu wengi huamini ya kwamba mabadiliko yaekolojia nahalihewa pamoja na kuchoka kwarutuba yaardhi yalisababisha kutoka kwa watu katika makazi ya awali.
Lakini ustaarabu huu uliona tena kipindi cha kustawi katika maeneo mengine hadi kuja kwa Wahispania. Miji mbalimbali ya Wamaya iliendelea kujitetea dhidi ya wavamizi naNojpeten, mji wa mwisho wa kujitegemea ulitekwa mwaka1696 tu.
Barabara ya mahekalu na piramidi ya jua mjini Teotihuacan
Teotihuacan ilikuwa mji mkubwa katika nyanda za juu, karibu na Mexico City ya leo. Kuanzia mwaka100 KK hadi takriban550 BK ilikuwa mji mkubwa wa Amerika, pia moja kati ya miji mikubwa duniani nakitovu chautamaduni kilichoathiri staarabu zote za Mexiko.
"Teotihuacan" ilikuwajina la Waazteki kwa mji huu, jina la kienyeji halikuhifadhiwa. Maana ya jina ni "mahali pa kuzaliwa kwamiungu". Wakati wamaendeleo yake mji ulikuwa na eneo lakilomita za mraba 30 ukiwa na wakazi angalau 150,000, labda hata 250,000 walioishi humo[4].
Hakuna uhakika ni akina nani waliojenga Teotohuacan. Mji wote ulipangwa kwa kufuatabarabara mbili zilizoelekea kaskazini-kusini na mashariki-magharibi. Hekalu kubwa na piramidi zinaonyesha umuhimu wadini, na mabaki yanyumba za wakubwa na watu wa kawaida yanaruhusu kupatapicha ya jamii iliyoishi hapa.
Teotohuacan ilikuwa kitovu chabiashara ya misafara ya mbali na pia ya elimu. Ukubwa wa mji unaonyesha kiwango cha juu chautawala naushirikiano kati ya watu wake.
Katikakarne ya 6 BK sehemu kubwa ya majengo iliharibika na kuchomwa. Hakuna uhakika kama hii ilikuwa tokeo la uvamizi kutoka nje au vurugu aumapinduzi ndani ya mji. Baada ya maharibio yale mji ulianza kurudi nyuma na idadi ya watu kupungua. Mnamo mwaka750 BK watu wote waliondoka: nimaghofu ya majengo makubwa tu yaliyobaki[5].
Kuanzia mwaka 1325 kabila laAzteki likaunda mji waTenochtitlan kwenye kisiwa chaziwa la Tezcoco. Waazteki wakaendelea kuunda milki kubwa lililoeena na kutawala sehmu kubwa ya nyanda za juu za Mexiko. Msingi wa milki yao ilikuwa ushirikiano na mji miwili jirani iliyounda mwungano wa pande tatu lakini Waazteki waliendelea kuwa mshiriki mkuu na mtawala wa Tenochtitlan hatimaye alikuwa mtawala mkuu. Walishambulia maeneo ya miji na makabila jirani na kuwalazimisha kulipa kadi kwao. Kama walikubali kutoa kodi kila mwaka na pia kushiriki katika vita za milki watawala wa kienyeji waliruhusiwa kuendelea na utawala wa ndani. Dini yao iliweka uzito kwa sadaka za binadamu waliochinjwa kwenye mahekalu ya miungu yao. Waliunda mfumo wa mikataba ya vita na milki nyingine ambako walikutana kwa mapigano yaliyo kubaliwa awali kwa shabaha ya kukamata wafungwa wengi iwezekanavyo na kuwatoa kama sadaka kwa miungu hekaluni baadaye.
Mwaka 1519 MhispaniaHernan Cortez alifika kwenye pwani la Mexiko. Katika miaka iliyofuata alifaulu kuendelea hadi mji wa Tenochtitlan akiongozana na kundi la Wahispania mamia kadhaa. Cortez aliweza kuungana na miji na makabila ya Waindio waliochoka utawala wa Azteki na kumpa askari za usaidizi. Mwaka 1520 waliingia Tenochtitlan kama wageni wa mfalmeMontezuma II wakaendelea kumkamata lakini baada ya kifo cha mfalme walifukuzwa wakakimbia kwa matatizo katika "usiku wa huzuni" (Kihisp.noche triste). Waazteki walidhoofishwa sana kutokana naepidemia ya ugonjwa wandui[6]. Cortez aliweza kukusanya jeshi kubwa la Waindio waliopinga Waazteki akavamia na kuharibu Tenochtitlan mwaka 1521 na kwenye magofu ya mji huu alianzisha mji mpya waMexico City (Kihisp.Ciudad de Mexico).
Mfano wauhuru wa Marekani mwaka1776 ulikuwa na athira pia kati ya wasomi wenyeji wa Mexiko. Jamii ya kikoloni iliundwa juu yaubaguzi kati ya Kreoli (walowezi wenye asili ya Hispania bila mchanganyiko na Waindio), Mestizos (asilimia kubwa ya wenyeji waliotokana nandoa zawanaume Wahispania nawanawake Waindio) na Waindio wenyewe. Lakini vyeo vyote vya juu, kama maafisa wa juu wa serikali, vilipatikana pekee kwa watu waliozaliwa Hispania na kutumwa Mexiko. Mawazo ya uhuru yalianza kupatikana kati ya Kreoli na Mestizos wa matabaka ya juu.
Katika Hispania Mpya (Mexico) kamati za miji kadhaa zilizoongozwa na Kreoli ziliapa kumfuata mfalme mfungwa halali pekee. Kamati Kuu ya Mexiko City ilitaka kuanzisha bunge la pekee kwa sababu Hispania haikuwa tena na serikali halali. Mfalme mdogo (gavana mkuu) alikubali. Viongozi wengine walitangaza ilhali mfalme halali hayuko tena sasa, nguvu yote iko mkononi mwa wananchi. Hapo Wahispania katika koloni walioshika vyeo vikuu waliamua kumpindua mfalme mdogo na kuwakamata viongozi wa Kreoli.
Uasi ulifaulu lakini vikundi vidogo vya wapinzani wa uhuru kutoka Hispania waliendelea kukutana nchini na kukusanya viongozi. Hatimayepadre KreoliMiguel Hidalgo y Costilla alikusanya jeshi lawanamgambowakulima Waindio na Kreoli akapigana na jeshi lililokuwa chini ya mamlaka ya maofisa Wahispania. Miguel Hidalgo alishindwa na kuuawa, lakini hii ilikuwa chanzo cha uasi mkubwa ambao Wakreoli na wakulima Waindio walipigana na jeshi lililofuata amri ya Wahispania katika koloni.
Mwaka kiongozi wa upande wa migambo ya uhuru Guerrero na jenerali wa jeshi la serikaliAgustin de Iturbide walikutana wakapatana kuungana. Vikosi vingi vya jeshi la kikoloni vilihamia upande wao. Gavana mpya aliyefika kutoka Hispania aliamua kukubali uhuru uliotangazwa tarehe28 Septemba1821. Iturbide alikuwarais wa kwanza na baadaye kwa kipindi kifupiKaisari wa Mexiko hadi kujiuzulu mwaka1823: hapo Mexiko ikaendelea kuwajamhuri.
Maeneo yaliyoongezwa, yaliyotengwa au kujitenga na Mexiko tangu uhuru wa mwaka 1821: A) Maeneo yaliyotwaliwa na Marekani (nyekundu, kichungwa, nyeupe), Chiapas kuchukuliwa kutoka Guatemala (buluu), eneo la Yucatan lililotwaliwa (nyekundu) na maeneo ya Shirikisho la Amerika ya Kati (zambarau).
Katika miaka iliyofuata nchi haikupata msimamo imara kisiasa wala kiuchumi. Serikali mara nyingi zilikuwa hafifu na kubadilishana.
Mwaka1835 Marekani ilijaribu kununua maeneo yaTexas naKalifornia lakini Meksiko ilikataa. Hata hivyo utawala wa Mexiko kuhusu maeneo haya ya kaskazini yake ulikuwa hafifu na wa juujuu tu, Waindio walijitegemea hali halisi nje ya miji michache. Hivyo serikali ya Mexiko ilikaribisha walowezi kutoka Marekani kuhamia Texas. Hao walowezi wenye utamaduni waKiingereza-Kimarekani walitangaza uhuru wao mwaka1836 wakaundaJamhuri ya Texas iliyochukuliwa na Marekani mwaka1845 kuwa jimbo lake.
Mexiko ilishambuliwa mara mbili naUfaransa kutokana na madai juu yamadeni ya taifa kwaraia aubenki za nje. Kwenyevita ya keki (1838-1839) Ufaransa ilidai fidia kwa uharibifu uliotokea katika duka la keki la Mfaransa mjini Mexiko namanowari za Ufaransa zilishambulia bandari za Mexiko hadi rais wake kukubali deni hili.
Mashambulio makubwa zaidi yalifuata mwaka1861. Mexiko ilishindwa kulipa madeni kwa mataifa ya nje. Ufaransa chini yaNapoleon III iliamua kufanya Mexiko nusu-koloni yake; jeshi la Ufaransa ilivamia nchi, kufukuza serikali na kumwekaMwaustriaMaximilian I kama "Kaisari wa Mexiko". Serikali ya raisBenito Juarez ilipinga uvamizi huu kwa njia ya vita ya wanamgambo na mwaka1866 Wafaransa walipaswa kuondoka tena, Maximilian aliuawa mwaka1867.
Utawala wa raisPorfirio Díaz uliendelea kwa miaka zaidi ya 30 na kuwasha moto yamapinduzi ya Mexiko alipojaribu kushinda tena kwa udanganyifu mwaka1910.
Miaka hadi 1921vita ya wenyewe kwa wenyewe iliharibu sehemu kubwa za nchi. Kuna makadirio ya kwamba wananchi milioni 1,5 (kati ya milioni 15) waliuawa na zaidi ya 200,000 walikuwawakimbizi, hasa kwenda Marekani[7].
Mwaka1917 katiba mpya ya nchi ilitolewa na mkutano wa bunge maalumu. Katiba hii ilikuwa katiba ya kwanza duniani kutangazahaki za kijamii. Hizo haki zililenga kutunza na kuboresha hali ya wananchi wenye maisha magumu kama wafanyakazi na wakulima dhidi yamabepari na wenye mashamba makubwa[8]. Katiba hii iliweka mamlaka nyingi mikononi mwa rais wa taifa anayechaguliwa na wananchi wote kwa kipindi kimoja cha miaka 6, halafu hawezi kuchaguliwa tena. Shabaha nyingine ya vifungu katika katiba ilikuwa kupunguza uwezo wa Kanisa Katoliki kuathiri siasa na jamii na hatimaye kukomeshaimani hiyo.
Siasa hii dhidi yaUkristo iliendelea chini ya rais Calles na kusababisha kipindi kingine cha vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka ya1926-1929. Katika mapigano hayo yaliyoitwaLa Cristiada wakulima wengi walichukua silaha kwa jina laKristoMfalme dhidi ya jeshi la serikali ili kuteteauhuru wa dini, wakipinga kufungwa kwamakanisa, kuzuiwaibada mbalimbali za hadhara na kuuawa kwa mapadre kamaMtakatifuKristofa Magallanes na wenzake. Vita hivyo vilisababisha vifo 250,000 na idadi hiyohiyo ya wakimbizi waliojisalimisha Marekani.
Baada ya mapinduzi mamlaka ilichukuliwa na Chama cha kitaifa cha mapinduzi (Partido Nacional Revolucionario PNR) kilichoendelea kutawala kwa miaka 71 kuanzia 1929 hadi2000.
Nchini wanaishi Wamarekani milioni 1, halafuwahamiaji wengine kutoka Amerika ya Kati,Lebanon, nchi nyingine zaAsia n.k. Kinyume chake, Wameksiko 13 milioni wako Marekani, na raia wengine 23 milioni wa nchi hiyo wana asili ya Meksiko.
Upande wadini walio wengi ni wafuasi waYesu Kristo katikaKanisa Katoliki (77.7%) aumadhehebu mengine (11.2%). Ni nchi ya pili duniani kwa wingi wa Wakatoliki, baada yaBrazil, na karibunusu kati yao wanashirikiibada kilawiki. Wasio na dini ni 8.1%.
↑Ndui ilikuwa ugonjwa iliyokuwa kawaida katika Ulaya wakati ule lakini ilikuwa ugonjwa mgeni kwa wenyeji wa Amerika ambao walikosa kinga dhidi yake; hivyo ilikuwa kati ya magonjwa wa kuambukizwa kutoka Ulaya yaiyoua Waindio wengi katika karne zilizofuata.
Levy, Santiago.Good intentions, bad outcomes: Social policy, informality, and economic growth in Mexico (Brookings Institution Press, 2010)
Meyer, Michael C., William L. Sherman, and Susan M. Deeds.The Course of Mexican History (7th ed. Oxford U.P., 2002)online editionIlihifadhiwa 2 Februari 2011 kwenyeWayback Machine.