
McKinsey & Company nikampuni ya kimataifa yaushauri wa masuala yausimamiziduniani. Inafanya uchambuzi wa kutathmini maamuzi ya usimamizi katika sekta za umma na za kibinafsi. McKinsey inachapishajarida laMcKinsey Quarterly tangumwaka wa1964, inafadhili shirika la utafiti lathe McKinsey Global Institute, linachapisha taarifa mbalimbali juu ya mada ya usimamizi, na linaandikavitabu vingi vya juu ya mada ya usimamizi.
McKinsey & Company ilianzishwaChicago ikiitwa James O. McKinsey & Company mwaka 1926 naJames O. McKinsey,profesa wa uhasibu katikaChuo Kikuu cha Chicago[1][2]ili kutumia kanuni zauhasibu kwenye mada ya usimamizi.
McKinsey alikufa mwaka wa1937, na kampuni hiyo ilirekebishwa mara kadhaa; McKinsey ya kisasa ilijitokeza mwaka1939.
Marvin Bower anachukuliwa kuwa ndiye aliyejengautamaduni na kanuni za McKinsey katikamiaka ya 1930 kulingana na uzoefu wake kamamwanasheria. Kampuni hii ndiyo ilianzisha sera ya "juu au nje", ambapo washauri ambao hawapandishwicheo wanaombwa kuondoka. McKinsey ilikuwa kampuni ya kwanza ya ushauri kuajiri wahitimu wa hivi karibuni wachuo, badala ya mameneja wazoefu.
Katikamiaka ya 1980 na1990, kampuni hiyo ilienea kimataifa. Ilikuwa nawafanyakazi 88 mwaka1951 na 7,700 mwanzoni mwa mwaka2000. Ushauri wa McKinsey umesaidia kuanzisha kanuni nyingi zinazotumika katikabiashara na kuchangia kwa mafanikio na pia kushindwa kwa mengi katika biashara katika zama za kisasa.
{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)| Makala hii kuhusu mambo yauchumi bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuMcKinsey& Company kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari. |