![]() | |||
Maelezo binafsi | |||
---|---|---|---|
Jina kamili | Mbwana Aly Samatta | ||
tarehe ya kuzaliwa | 23 Desemba1992 (1992-12-23) (umri 32) | ||
mahali pa kuzaliwa | Dar es Salaam,Tanzania | ||
Maelezo ya klabu | |||
Klabu ya sasa | PAOK | ||
Senior career* | |||
Miaka | Timu | Apps† | (Gls)† |
2010–2011 | Simba | 25 | (13) |
2011–2016 | TP Mazembe | 103 | (60) |
2016–2020 | Genk | 144 | (56) |
2020– 2020 | Aston Villa | 14 | (1) |
2020 - 2023 | Fernabahce | 30 | (5) |
2021 - 2022 | →Antwerp (mkopo) | 32 | (5) |
2021 - 2022 | →Genk (mkopo) | 33 | (6) |
2023 - | →PAOK | 30 | (2) |
Timu ya Taifa ya Kandanda‡ | |||
– | Tanzania | 81 | (22) |
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only. † Appearances (Goals). |
Mbwana Ally Samatta, (alizaliwa23 Disemba1992), nimchezaji wampira wa miguu waTanzania katikaklabu ya Feberbahce nchiniUturuki[1]. Mbwana ninahodha watimu ya taifa ya TanzaniaTaifa Stars na kabla ya kuhamia klabu ya Feberbahce (Uturuki) alikuwa akucheze timu ya Aston Villa nchiniUingereza[2].
Samatta alianza kucheza soka la kulipwa katika klabu yaAfrican Lyon F.C. mwaka2008 nchiniTanzania. Alisajiliwa na klabu yaSimba mwaka2010, ambapo alicheza katika nusu msimu tu kabla ya kujiunga na klabu yaTP Mazembe yaJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Alicheza kwa miaka mitano ndani ya TP Mazembe na kujijengea nafasi katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo.
Mwaka 2015, alishinda taji la mchezaji bora wa mwaka waAfrika, na kumaliza msimu akiwa mfungaji bora wa mashindano ya klabu bingwa Afrika (Ligi ya Mabingwa Afrika) na kuisaidia klabu yake kushinda taji hilo.
Samatta alijiunga na klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji mnamo januari2016, aliisaidia kufuzu michuano yaUlaya maarufu kama Europa Ligi na kushinda taji la ligi ya Ubelgiji (Belgian Jupiler Ligi mwaka2019. Alimaliza msimu akiwa mfungaji bora wa ligi hiyo akashinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Ubelgiji (Ebony Shoe award)[3].
Manamo Januari mwaka 2020, Samatta alisajiliwa na klabu yaAston Villa ya nchini Uingereza na kuwa mchezaji wa kwanza kutoka nchini Tanzania kucheza na kufunga goli ligi kuu ya nchini Uingereza.
Samatta alikua mchezaji muhimu waTP Mazembe waliposhinda taji la klabu bingwa Afrika mwaka 2015 (2015 CAF Champions Ligi), akifunga jumla ya magoli saba na kumaliza akiwa mfungaji bora.[4]
Mnamo Januari 2016, aliposhinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutokeaAfrika ya Mashariki kutwaa tuzo hiyo. Katika ugawaji wa tuzo hizo uliofanyika jijiniAbuja,Nigeria, tarehe 7 Januari 2016, Samatta alikusanya jumla ya alama 127, akimzidi mchezaji mwenzakeRobert Kidiaba mlinda lango wa TP Mazembe na timu ya taifa ya DR Congo aliyepata alama 88.Baghdad Bounedjah raia waAlgeria alishika nafasi ya tatu akiwa na alama 63.[5] Katika mchezo dhidi yaMoghreb Tétouan yaMoroko, Samatta alifunga magoli matatu kwa mpigo (hat-trick) yaliyowafanya wasonge hatua yanusu fainali ya klabu bingwa Afrika. Magoli hayo yanakumbukwa sana katikahistoria ya klabu ya TP Mazembe.[6]
Muda mfupi baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika, alijiunga na klabu ya K.R.C. Genk kwa mkataba wa miaka minne na nusu.[7] Tarehe 23 Agosti 2018 Samatta alifunga goli tatu kwa mpigo(hat-trick) dhidi ya Brøndby IFkwenye mashindano ya Ulaya maarufu kwa jina la Europa Ligi walfanikiwa kupata ushindi wa goli 5–2.[8]Mei 2019 aliishinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Ubelgiji (Ebony Shoe).
Mnamo Januari 20, 2020, Samatta alijiunga na klabu yaAston Villa inayoshiriki ligi Kuu ya Uingereza kwa mkataba wa miaka minne na nusu.[9] Uhamisho huu ulimfanya Samatta kuwa mchezaji wa kwanza wa kitanzania kucheza ligi kuu ya Uingereza.[10] Ada ya uhamisho inakadiriwa kuwa £8.5 milioni.[11][12] Mchezo wa kwanza alicheza siku nane baada ya kusajiliwa dhidi ya Leceister City kwenye mzunguku wa pili wa mashindano ya Carabao hatua ya nusu fainali, waliibuka na ushindi wa magoli 2 – 1, kwa matoke ohayo, Villa walifika hatua ya fainali.[13]
Samatta alifunga goli lake la kwanza manamo 1 Februari 2020, walipocheza naBournemouth, mchezo ulimalizika kwa Villa kushinda magoli 2 - 1. Goli hilo lilimfanya Samatta kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kucheza na kufunga kwenye mashindano ya Ligi ya Uingereza.[14]
Samatta alijiunga na Klabu ya Fernabahce ya nchini Uturuki tarehe 25 Septemba 2020, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.[15] Ulipofika mwisho wa mkopo mnamo Julai 2021, Samatta alisaini mkataba wa miaka minne, hii ilikua ni sehemu ya makubaliano ya uhamisho wake.[16]
Tarehe 1 Septemba 2021, Samatta alijiunga naRoyal Antwerp ya nchini Ubelgiji kwa mkopo wa msimu mzima.[17]
Ilipofika 16 Agosti 2022, Samatta alirudi tena Genk kwa mkopo, uhamisho huo ulikua na chaguo la Genk kumnunua.[18]
Mnamo tarehe 17 Julai 2023, timu ya nchini UgirikiPAOK ilitangaza kumsajili Samatta kwa mkataba wa miaka miwili, mkataba huo ulikua na nafasi ya kuongeza mwaka mmoja.[19]
Mbwana Samatta niMndengereko kutokaKibiti kwakabila. Katika maisha yaimani niMuislamu.[20]
Klabu | Msimu | Ligi | Cup | Kombe la ligi | Ya Bara | Mengineyo | Jumla | Ref. | |||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Ushindani | Michezo | Magoli | Michezo | Magoli | Michezo | Magoli | Michezo | Magoli | Michezo | Magoli | Michezo | Magoli | |||
Simba S.C. | 2010–11 | Ligi Kuu Tanzania Bara | 25 | 13 | — | [tanbihi 1] | 2 | — | 25 | 15 | [21][22] | ||||
TP Mazembe | 2011 | Linafoot | 8 | 2 | — | — | 8 | 2 | [21][22] | ||||||
2012 | 29 | 23 | — | 9 | 6 | — | 37 | 29 | [21][22] | ||||||
2013 | 37 | 20 | — | 5Hitilafu ya kutaja: Invalid<ref> tag; refs with no name must have content | 5 | — | 42 | 25 | [21][22] | ||||||
2013–14 | 29 | 15 | — | 8 | 4 | — | 37 | 19 | [21][22] | ||||||
2014–15 | — | 6 | 4 | — | 6 | 4 | [22] | ||||||||
2015–16 | — | 6 | 4 | — | 6 | 4 | [22] | ||||||||
Jumla | 103 | 60 | 0 | 0 | 33 | 23 | 0 | 0 | 136 | 83 | – | ||||
K.R.C. Genk | Ligi kuu ya Ubelgiji | 6 | 2 | 0 | 0 | — | — | 12[tanbihi 2] | 3 | 18 | 5 | [23] | |||
2016–17 | 27 | 10 | 4 | 2 | — | 18 | 5 | 10[tanbihi 2] | 3 | 59 | 20 | [23] | |||
2017–18 | 20 | 4 | 4 | 0 | — | — | 11[tanbihi 2] | 4 | 35 | 8 | [23] | ||||
2018–19 | 28 | 20 | 1 | 0 | — | 12 | 9 | 10[tanbihi 2] | 3 | 51 | 32 | [23] | |||
Jumla | 81 | 36 | 9 | 2 | 0 | 0 | 30 | 14 | 43 | 13 | 163 | 65 | – | ||
Jumla maisha ya soka | 209 | 109 | 9 | 2 | 0 | 0 | 63 | 39 | 43 | 13 | 324 | 163 | – |
Taifa Stars | ||
Mwaka | Michezo | Magoli |
---|---|---|
2011 | 9 | 2 |
2012 | 4 | 0 |
2013 | 10 | 6 |
2014 | 3 | 1 |
2015 | 7 | 2 |
2016 | 4 | 1 |
2017 | 3 | 3 |
2018 | 5 | 2 |
2019 | 6 | 1 |
Total | 51 | 18 |
Goli | Tarehe | Uwanja | Mpinzani | Alama | Matokeo | Mashindano |
---|---|---|---|---|---|---|
1. | 26 Machi 2011 | Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam, Tanzania | ![]() | 2–1 | 2–1 | kufuzu AFCON 2012 |
2. | 3 Septemba 2011 | ![]() | 1–0 | 1–1 | ||
3. | 11 Januari 2013 | Uwanja wa Adis ababa,Addis Ababa, Ethiopia | ![]() | 1–1 | 1–2 | Mchezo wa Kirafiki |
4. | 6 Februari 2013 | Uwanja wa Taifa Dar es Salaam | ![]() | 1–0 | 1–0 | |
5. | 24 Machi 2013 | ![]() | 2–0 | 3–1 | kufuzu fainali za kombe la dunia 2014 | |
6. | 3–0 | |||||
7. | 4 Disemba 2013 | Uwanja wa Afraha,Nakuru, Kenya | ![]() | 1–0 | 1–0 | hatua ya makundi mashindano ya CECAFA 2013 |
8. | 12 Disemba 2013 | uwanja wa Nyayo,Nairobi, Kenya | ![]() | 1–1 | 1–1 | mashindano ya CECAFA hatua ya mtoano 2013 |
9. | 3 Agosti 2014 | uwanja wa Estádio do Zimpeto,Maputo, Msumbiji | ![]() | 1–1 | 1–2 | Kufuzu AFCON 2015 |
10. | 7 Oktoba 2015 | Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Tanzania | ![]() | 1–0 | 2–0 | kufuzu fainali za kombe la dunia 2018 hatua ya kwanza |
11. | 14 Novemba 2015 | ![]() | 2–0 | 2–2 | kufuzu fainali za kombe la dunia 2018 – hatua ya pili | |
12. | 23 Machi 2016 | uwanja wa Stade Omnisports Idriss Mahamat Ouya,N'Djamena, Chad | ![]() | 1–0 | 1–0 | kufuzu AFCON 2017 hatua ya makundi |
13. | 25 Machi 2017 | Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Tanzania | ![]() | 1–0 | 2–0 | Mchezo wa kirafiki |
14. | 2–0 | |||||
15. | 10 Juni 2017 | ![]() | 1–0 | 1–1 | kufuzu AFCON 2019 Kundi L | |
16. | 27 Machi 2018 | ![]() | 1–0 | 2–0 | Mchezo wa kirafiki | |
17. | 16 Oktoba 2018 | ![]() | 2–0 | 2–0 | kufuzu AFCON 2019 | |
18. | 27 Juni 2019 | uwanja wa 30 June Stadium,Cairo, Misri | ![]() | 2–1 | 2–3 | AFCON 2019 Kundi C |
19. | 8 Septemba 2019 | Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Tanzania | ![]() | 1–0 | 1–1 (3–0 mikwaju ya penalti) | kufuzu michano ya kombe la dunia 2022 hatua ya kwanza |
TP Mazembe[24]
Genk
Binafsi
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: url-status (link){{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite news}}
:More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link){{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link){{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)![]() | Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuMbwana Samatta kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari. |
Hitilafu ya kutaja:<ref>
tags exist for a group named "tanbihi", but no corresponding<references group="tanbihi"/>
tag was found