Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Mbeya (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jiji la Mbeya
Jiji la Mbeya is located in Tanzania
Jiji la Mbeya
Jiji la Mbeya

Mahali pa mji wa Mbeya katika Tanzania

Majiranukta:8°53′24″S33°25′48″E / 8.89000°S 33.43000°E /-8.89000; 33.43000
NchiTanzania
MkoaMbeya
WilayaMbeya Mjini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla541,603
Mkowa wa Mbea

Jiji la Mbeya nimji mkubwa kusini-magharibi mwaTanzania wenye hadhi yajiji namsimbo wa Posta 53100.

Mbeya nikitovu chaNyanda za Juu za Kusini ambazo ni eneo lauzalishaji wamazao mengi.

Nimakao makuu yamkoa wa Mbeya.

Jiografia

[hariri |hariri chanzo]

Mji umeenea katikabonde kati yasafu zamilima ya Mbeya namilima ya Uporoto.Mlima mkubwa unaoonekana kutoka mjini niMlima wa Mbeya (Mbeya Peak) wenyeurefu wam 2818.

Eneo la mji ni kati ya m 1600 kitovuni na m 1900 au zaidi juu yaUB kwenye mitelemko yamlima Loleza.

Hali ya hewa hainajoto kali kutokana nakimo. Wakati wa Juni-Julaihalijoto wakati wausiku inaweza kushuka chini hadi 0°C, mlimani hata chini zaidi.

Mvua zinaanzamwezi Novemba hivyo ni wakati wa kupanda. Kwa kawaida mvua zinasimama tena Januari-Februari na kunyesha kwa wingi Machi-Aprili.

Uti wa mgongo wa mji nibarabara kuu yaTANZAM inayounganisha sehemu za nje kati yaUyole naMbalizi.

Kitovu kipya cha mji kinahamishwa kwendakata yaForesti iliyoko kando ya barabara kuu.

Station Road huko Mbeya sehemu ya kale ya mjini.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Jina la Mbeya limetokana naneno laKisafwa "Ibheya" ambayo maana yake nichumvi, kwani miaka mingiwafanyabiashara walikuwa wanafika mahali hapo kubadilishana mazao yao kwa chumvi.

Mlima mkubwa ulio karibu ulijulikana kwa jina la "Mbeya"[1] wakati waukoloni wa Kijerumani, na mji ulipokea baadaye jina kutokana na mlima huu.

Mji wa kisasa wa Mbeya ulianzishwa nawakoloniWaingereza mnamo mwaka1927. Wakati uledhahabu ilianza kupatikana mlimani karibu na Mbeya hadiChunya.

Historia inavyoonekana katika jiografia ya Mbeya

[hariri |hariri chanzo]

Mji ulianzishwa katika sehemu zinazoitwa bado Uhindini, Uzunguni na Majengo. Mji ulipangwa kufuatana na kawaida ya miji wa kikoloni yaAfrika ya Mashariki kuwa na sehemu tatu:

Makanisa ya kale kama ishara ya historia

[hariri |hariri chanzo]

Mahali pamakanisa ya kale panaonyesha ugawaji huu wa kihistoria:

  • Kanisa laAnglikana lililokuwadhehebu rasmi laUingereza lipo chini ya Uzunguni na karibu na ofisi za kiserikali (zinazoelekea siku hizi kuhamishwa kwendaForesti) kamaMkuu wa Mkoa na mahakama. Kanisa hili nijengo dogo kwa sababu lilipangwa kwa kundi dogo la maafisa na wafanyabiashara pamoja nawakulima Waingereza wa Mbeya.
  • Kanisa la mjini laMoravian, ambalo ni dhehebu laKikristo asilia la Mbeya liko Majengo iliyokuwa sehemu kwa Waafrika. Kati ya Waingereza hawakuwepo Wamoravian.
  • Kanisa KuuKatoliki lilihudumia Wazungu wachache, hasaWaeire, kati ya wakoloni pamoja na Wahindi kutokaGoa na pia Waafrika: kwa hiyo iko kati ya Uzunguni na Uhindini karibu na Majengo.

Mji uliendelea kupanuka pande zote. Barabara kuu yaTANZAM inaunganisha sehemu za nje kati ya Uyole na Mbalizi.

Siku hizi sehemu kubwa ya wakazi ni Wakristo, hasa wafuasi waKanisa Katoliki,Kanisa la Moravian naKanisa la Kilutheri. Makundi makubwa mjini niWasafwa (wenyeji) naWanyakyusa waliohamia kutokaRungwe. Wanyakyusa ndio waliotangulia kuleta Ulutheri mjini.

Kuna piamsikiti mkubwa nahekalu laWahindu.

Mawasiliano

[hariri |hariri chanzo]
Kituo cha reli ya TAZARA Mbeya
Treni ya TAZARA kwenye kituo Mbeya

Mbeya ninjiapanda yanjia mbalimbali muhimu: Barabara kuu yalami kutokaDar es Salaam (km 850) hugawanya hapa kwendaMalawiMsumbiji kupitiaTukuyu/Rungwe, na kwendaZambiaAfrika Kusini kupitiaTunduma/Mbozi.

Vilevile njia yareli yaTAZARA hupita Mbeya kuelekea Zambia. Kunaghala kubwa kwa ajili ya mizigo ya Malawi inayofikishwa kwa reli kutoka Dar es Salaambandarini ikihamishwa kwamalori kwenda Malawi.

Mbeya imekuwa nauwanja wa ndege mdogo usiokuwa nahuduma ya kawaida kwa muda mrefu. Lakini kuna mipango ya kujenga uwanja mpya hukoSongwe zipatazo km 40 kufuata njia ya kwenda Zambia.

Tangumiaka ya 1990 kitovu cha mji kinahamishwa kutoka eneo la zamani kwenda karibu na barabara kuu ya Dar es Salaam – Zambia.

Wakazi

[hariri |hariri chanzo]

Mbeya ni mji wa nne kwa ukubwa nchiniTanzania.Idadi ya wakazi imehesabiwa kuwa 385,279 katikasensa yamwaka 2012. Katikasensa ya mwaka2022 walihesabiwa 541,603[2]. Wengine 300,000 hivi wanaishi katika mazingira karibu na Mbeya mjini.

Kwa asili Mbeya ilikuwa eneo laWasafwa. Siku hizi sehemu kubwa ya wakazi wanaweza kuwa mchanganyiko wa Wasafwa pamoja na makabila yaWanyakyusa kutoka wilaya zaRungwe naKyela,Wanyiha kutokaMbozi,Wandali kutokaIleje naWakinga kutokaMakete.

Uchumi

[hariri |hariri chanzo]

Uchumi wa Mbeya mjini umetegemeakilimo cha mazingira yake na biashara.

Viwanda mbalimbali vilianzishwa, lakini havikufaulu sana. Kuna viwanda kwa mfanoZana za kilimo, Highland Soap, Mbeya Textiles. Mbeya Ceramics iliporomoka kitambo.

Elimu

[hariri |hariri chanzo]

Pamoja nashule za sekondari kunataasisi kadhaa zaelimu ya juu kama vile:

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. Wajerumani waliandika "Mbeja" wakitamka "j" kama "y", linganishaKamusi ya Koloni za Kijerumani, makala "Usafua"
  2. https://www.nbs.go.tz

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Kata za Jiji la Mbeya -Tanzania

ForestGhanaIdudaIganjoIganzoIgawiloIlemiIlombaIsangaIsyesyeItaganoItendeIteziItijiIwambiIyelaIyungaIziwaKalobeMaangaMabatiniMaendeleoMajengoMbalizi RoadMwakibeteMwasangaMwasenkwaNondeNsalagaNsohoNzovweRuandaSindeSisimbaTembelaUyole


Makala hii kuhusu maeneo yaMkoa wa Mbeya bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuMbeya (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Mbeya_(mji)&oldid=1308322"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp