Mawese nimafuta ya kula yanayotolewa katikamatunda yamti wamchikichi (Elaeis guineensis). Ni mafuta ya kupikia yaAfrika, hasa penye asili ya mchikichi kutokana na kupatikana kwa wingi katika nchi za kanda yaGuinea.
Kuna aina mbili za mawese; mawese hasa hutolewa na nyama ya tunda, inaranginyekundu navitamini nyingi. Inatumika kama mafuta ya kupikia ama moja kwa moja ikitolewa nawakulima wenyewe na kuonyesha rangi nyekundu. Kama mawese inatengenezwakibiasharakiwandani rangi inaondolewa kwa njia ya kusafisha mafuta kwenye vichujio. Baada ya kusafishwa huwekwa kwenyemakopo auchupa na kuuzwamadukani au kupelekwa nje. Mafuta haya yanatumika pia viwandani kwa kutengeneza majarini,sabuni,mishumaa, mafuta ya kupakaa mwilini na aina mbalimbali ya madawa na urembaji.
Mawese hutumika piakiteknolojia tangu miaka ya nyuma kwa kutengenezadizeli. Hasa nchiniMalaysia teknolojia hii imesonga mbele. Malaysia inajaribu kupunguzagharama za kununuapetroli nadizeli kwa kutengeneza kiwanda kikubwa cha kusafisha mawese kuwa dizeli.Sheria ya Malaysia inadai kuanzia mwaka2007 ya kwamba dizeli yote inayouzwa nchini iwe na 5% dizeli ya mawese.
Aina ya pili ni mafuta yanapatikana katika kiini cha tunda. Haya baadhi ya wenyeji huyaita mafuta ya mise. Mafuta haya yanahalijoto ya kuyeyuka kwenye 26 – 28C°. Hivyo kwa kawaida ni imara, si majimaji. Inatumika katika viwanda vya vyakula lakini pia kwamajarini. Yanatumika pia sana katika madawa ya urembaji na madawa ya kusafishia. Hata viwanda vya kutengenezaalumini hutumia aina hii ya mawese. Kuna biashara kubwa ya viini vya mchikichi (mise) kwa sababu husafirishwa bila kuharibu mafuta ndani yake.
Kiuchumi kwa nchi za Afrika ya Magharibi biashara ya mawese ilichukua nafasi yabiashara ya watumwa; hadi mwanzo wa karne ya 19 falme za pwani zilitajirika kwa kuwauziawafanyabiasharaWazunguwatumwa kwa ajili ya masoko yaAmerika.
Biashara hii ya watumwa ilipigwa marufuku polepole. Mabadiliko ya sheria katikaUingereza yalitangulia. Mapatano ya kimataifa kwenyeMkutano wa Vienna mwaka1815 yalipakana biashara hii ikapungua hadi kwisha.
Umuhimu mpya wa Afrika ya Magharibi kwa ajili ya Ulaya ulikuwa mafuta ya mawese. Hasa viini vilipelekwa Ulaya kwa sababu mawese asilia huharibika haraka. Kabla ya kuwepo kwa viwanda Afrika kwenyewe viini viliweza kusafirishwa mbali bila kuharibu mafuta ndani yake. Mawese ya tunda lenyewe linaharibika kama haitengenezwi kwa kufuatambinu mbalimbali zinazopatikana kiwandani lakini si rahisi kuzitumia katikauzalishaji wa kienyeji.